HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 7, 2023

NEMC YAWATAKA WACHIMBAJI WA MADINI WANAOMILIKI MABWAWA YA TOPE SUMU KUFANYA UKAGUZI

Mkurugenzi mkuu Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira –NEMC, Dkt Samuel Gwamaka limewataka wachimbaji wa madini wakubwa na wakati wanaomiliki mabwawa ya tope sumu kufanya ukaguzi hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam katika kikao chake na wanahabari ambapo amesema ukaguzi huo ujiekeleze katika kubaini viashiria vya hatari lengo ni kudhibiti majanga kabla hayajaleta madhara kwa jamii na mazingira.

Amesema serikali haitavumilia kuona viashiria chochezi dhidi ya mazingira na jamii kwa ujumla hivyo wamiliki wa mabwawa ya tope sumu katika migodi wanapaswa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika kipindi hiki mvua zikiendelea kuntesha.

"Haya mabwawa tulionayo ni yamaeneo yanayochukuwa ardhi kubwa na tope kubwa lenye sumu kwenye migodi mikubwa tuliyonayo, sasa kunapotokea mvua kubwa kupita wastani mabwawa huwa yanajaa kupita uwezo wake kwa hiyo ni lazima tuchukuwe tahadhari" amesema Dkt. Gwamaka

Katika hatua nyingine Dkt. Gwamaka amesema NEMC imetoa kipindi cha mwezi mmoja Novemba 7 kwa wazalishaji wa vinywaji vya energy vinavyotumia chupa za rangi kuweka mpango wa kurejeleza chupa hizo ili kuhifadhi mazingira na watakaoshindwa kutekeleza azigo hilo la kisheria watafungiwa kuzalisha kinywaji hicho ili kulinda mazingira.

Chupa za rangi zinazozalishwa vinywaji vya energy zimekuwa zikilalamikiwa kuchafua mazingira kutokana na kutookotwa kwa ajili ya kufanyiwa urejeleshaji hivyo utekelezaji wa tamko la NEMC utakapoanza utakwenda kumaliza tatizo hilo.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad