HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 9, 2023

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA LAPONGEZA UFANISI KLINIKI YA ARDHI


Na. Dennis Gondwe, DODOMA

Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amepongeza ufanisi wa Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini hapa na kusema ni mafanikio makubwa.

Pongezi hizo alizitoa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya kwanza uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.

Prof. Mwamfupe ambae ni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “kniliki hiyo ni muendelezo wa mafanikio katika sekta ya Ardhi. Jana pekee zimetolewa hati 217, zikijumuisha maombi yaliyopokelewa papo kwa hapo. Tuendelee kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha kliniki hii”.

Katika hatua nyingine, Prof. Mwamfupe ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ya Fedha na Utawala alimteua Diwani wa viti maalum, Rosemary Nitwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala.

“Waheshimiwa madiwani, mtakumbuka Mheshimiwa Grace Milinga alikuwa mmoja wetu hapa akiwa Diwani na alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala na alijiuzuru nafasi hiyo. Naomba mridhie kuteuliwa kwa Mheshimiwa Rosemary Nitwa kuziba pengo hilo” aliomba Prof. Mwamfupe na madiwani kuridhia.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad