HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 30, 2023

Twiga kidedea tuzo ya juu ya kuchangia pato la Serikali

Waziri wa Madini wa Malawi, Mh.Monica Chang'anamuno (Kushoto) akikabidhi tuzo ya juu ya kuchangia pato la Serikali kwa Afisa Mawasiliano wa Twiga Minerals Corporation, Abella Mutiganzi (katikati) kwa niaba ya kampuni wakati wa hafla ya usiku wa madini iliyofanyika jijini Dar es Salaam karibuni, (kulia) ni Waziri wa Madini, Mh. Antony Mavunde.Twiga pia ilishinda tuzo maalum ya umiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini (Special Mining License Holder Awards).
Afisa Mawasiliano wa Twiga Minerals Corporation, Abella Mutiganzi (katikati) akiwa na Mawaziri wa Madini wa Malawi na Tanzania baada ya kupokea tuzo hiyo.
Tuzo ambazo Twiga imetunukiwa katika hafla ya Usiku wa Madini
---
Ubia wa Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga na kampuni ya Dhahabu ya Barrick, unazidi kuleta mafanikio mbalimbali ambapo katika hafla ya usiku wa madini iliyofanyika karibuni, Twiga imefanikiwa kushinda tuzo ya juu ya kuchangia pato la Serikali pia ilishinda tuzo maalum ya umiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini (Special Mining License Holder Awards) .Tuzo hizo zilitolewa na Wizara ya Madini ambayo iliandaa hafla hiyo.

Tuzo hizo zilikabidhiwa na Waziri wa Madini wa Malawi, Mh.Monica Chang'anamuno, kwa kushirikiana na Waziri wa Madini Mh.Antony Mavunde, ambaye alipongeza Twiga kwa kuendelea kufanikisha kuleta mapinduzi makubwa ya maendeleo nchini kupitia uwekezaji katika sekta ya madini kupitia migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.

Tangu mwaka 2019 ilipoichukua migodi hiyo iliyokuwa imekufa, Barrick Imeibadilisha na kuifanya kuwa na viwango vya kimataifa, vilevile kampuni kipindi hicho kampuni imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika uchumi wa Tanzania ambapo mwaka huu Twiga ilitambuliwa kuwa mlipaji mkubwa wa gawio kuliko makampuni yote ambayo Serikali ina maslahi nayo.

Migodi ya Barrick pia hutumia asilimia 84 ya bajeti yake ya manunuzi kwa makampuni ya ndani huku asilimia 96 ya nguvu kazi yake ikiwa ni ya wananchi wa Tanzania.

Kupitia sera ya Uwajibikaji Kwa jamii (CSR) kampuni imeishatuimia kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 13.2 kutekeleza miradi ya kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi katika sekta mbalimbali ikiwemo kuboresha elimu, Afya, Miradi ya maji Safi, Na kuimarisha miundombinu ya barabara. Miradi hiyo imefanikisha kuleta ubora wa maisha katika jamii zinazozunguka migodi yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad