HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 30, 2023

HALOTEL TANZANIA YAZINDUA KAMPENI YAKE MPYA,KUWAUNGANISHA WATANZANIA KUPATA HUDUMA BORA


·        Miaka 8 ya Halotel, Wateja zaidi ya 1000 kushinda zawadi KemKem

 Halotel Tanzania kampuni iliyoenea maeneo mengi nchini inayo furaha kuzindua kampeni yake Mpya ya kusherehekea miaka 8 tangu kuanza kutoa huduma za mawasiliano, ambayo imepewa jina la "Kivumbi na Halotel." Tukio hili muhimu linaadhimisha miaka 8 ya kuwaunganisha watanzania katika huduma bora za Mawasiliano kuanzia Vijijini mpaka Mjini. Hii ni sehemu ya shukrani kwa wateja wake wa thamani. Promosheni ya "Kivumbi na Halotel," imesheheni zawadi ambazo zinahakikisha kwamba miaka nane ya Halotel ni ya kipekee kama ilivyo safari yenyewe.

Kama sehemu ya sherehe hii ya miaka 8, wateja wa Halotel wana nafasi ya kushinda zawadi kemkem jumla ya 1,510 katika kampeni ya "Kivumbi na Halotel." Halotel itatoa zawadi mbalimbali kila wiki. Zawadi hizo zinajumuisha simu janja ya mkononi aina ya Samsung Galaxy A 34 5G ikiwa pamoja na laini ya Halotel yenye data ya GB 5 bure. Simu janja ya mkononi ya Samsung Galaxy M14 na laini ya Halotel yenye data ya GB10 bure. Routers za Halotel pamoja na laini Halotel yenye data ya GB5 bure ili kuboresha matumizi bora ya mtandao wa intaneti kwa wateja mahali popote na vifurushi vingine vingi vya kufurahia faida zaidi kutoka kwa huduma za Halotel.

Zawadi kubwa kuliko na ya kusisimua ni gari jipya aina ya Mazda CX5, moja ya magari yenye mtindo wa kipekee sokoni. Zawadi hii itatolewa mwishoni mwa Promosheni kwa mteja atakayebahatika kushinda.

Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana na inapatikana kwa wateja wote wa Halotel. Ili kushiriki, wateja wanatakiwa kununua vocha ya kukwangua au kwa Halopesa yenye thamani ya TZS 2,000 au zaidi. Au Kujiunga kifurushi cha huduma chenye thamani ya kuanzia TZS 2,000 au zaidi kwa salio la kawaida au kupitia huduma ya Halopesa ya Halotel.

Promosheni ya "Kivumbi na Halotel" inalenga na kuzingatia wateja wote wa Halotel walioko nchi nzima. Lengo kuu likiwa ni kutoa shukrani kwa watanzania na wateja wao kwa ujumla kwa kuendelea kuunga mkono na kuchagua mtandao wa Halotel kwa mahitaji yao ya mawasiliano kwa miaka 8 sasa.

Bwana Patric Rwegoshora, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Halotel, alielezea shauku yake kuhusu sherehe ya miaka 8 na kampeni hii ya "Kivumbi na Halotel," kwa wateja, akisema, "Halotel, tunatambua kwamba mafanikio yetu hayawezi kutenganishwa na imani, uaminifu, wa wateja wetu kutumia mtandao wetu. Ni kwa shukrani kubwa tunasherehekea miaka 8 ya ufanisi wa mawasiliano nchini Tanzania. Promosheni hii, ya 'Kivumbi na Halotel,' ni moja njia yetu ya kusema 'asante' kwa wateja wetu kwa kuendelea kuwa nasi. Tunawakaribisha na tutatamani kuona wateja wengi iwezekanavyo wanashiriki na kushinda zawadi za hizi"

Wateja wanahimizwa kushiriki kikamilifu na kutumia fursa hii adhimu ya kushinda zawadi mbalimbali na huku wakitengeza nafasi ya kushinda zawadi kubwa kuliko ya gari Moya aina ya Mazda 5CX kutoka Halotel kupitia kampeni hii itakayodumu kwa miezi mitatu kuanzia Oktoba 2023, hivyo nafasi za kushinda ni nyingi kwa kushiriki zaidi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu promosheni ya maadhimisho ya miaka nane (08) ya Halotel,wateja wanaweza tembelea tovuti yetu ya www.halotel.co.tz

Pia, unaweza kutufikia kupitia mitandao ya kijamii ya Halotel Instagram (Halotel_tanzania) na Facebook (Halotel Tanzania), au wasiliana na timu yetu ya huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 100..

Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Halotel Patrick Rwegoshora’ (kushoto) akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya wateja yenye jina la “Kivumbi Na Halotel” uliofanyika jijini Dar es salaam. Promosheni hii ni mwendelezo wa kuadhimisha miaka nane (08) ya kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini. 

Ili Mteja wa Halotel aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kuweka vocha ya kukwangua au Kwa Halopesa yenye thamani kuanzia Shilingi 2000 na zaidi au kujiunga kifurushi cha huduma chenye thamani kuanzia Shilingi 2,000 au zaidi kwa salio la kawaida au Kupitia Halopesa itakayomuwezesha kuingia kwenye droo na kuweza kuibuka mshindi wa zawadi mbalimbali kubwa kuliko ikiwa ni gari mpyaa kabisa aina ya Mazda CX5. Pamoja naye ni Afisa Masoko huduma za Kifedha za Halopesa Roxana Kadio.


Afisa Masoko wa Huduma za Kifedha za HaloPesa (kulia) akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya wateja yenye jina la “Kivumbi Na Halotel” uliofanyika jijini Dar es salaam. Promosheni hii ni mwendelezo wa kuadhimisha miaka nane (08) ya kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini. 

Ili Mteja wa Halotel aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kuweka vocha ya kukwangua au Kwa Halopesa yenye thamani kuanzia Shilingi 2,000 na zaidi au kujiunga kifurushi cha huduma chenye thamani kuanzia Shilingi 2,000 au zaidi kwa salio la kawaida au Kupitia Halopesa itakayomuwezesha kuingia kwenye droo na kuweza kuibuka mshindi wa zawadi mbalimbali kubwa kuliko ikiwa ni gari mpyaa kabisa aina ya Mazda CX5. Pamoja naye ni Mkuu wa Kitengo Cha Huduma Kwa wateja Halotel Patric Rwegoshora. 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad