HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 30, 2023

NAIBU KATIBU MKUU POSSI AISHUKURU ICAO KWA KUKAMILISHA MRADI WA UIMARISHAJI NA UDHIBITI WA USAFIRI WA ANGA

 


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi ameshukuru Shirika la Anga Duniani (ICAO) kwa kukamilisha mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga ambao uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China uliogharimu takriban Dola Milioni Moja.

Dkt. Possi amesema hayo alipomuwakilisha Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika kikao kazi cha kuhitimisha mradi huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imehakikisha utekelezaji wa mradi huu umefanyika katika muda uliopangwa na kwa viwango vilivyotakiwa na sasa sekta ya Usafiri wa Anga nchini utaendelea kuimarika maradufu”
aliongeza Dkt Possi.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian ameelezea kuridhishwa na hatua za utekelezwaji wa mradi huu na kusisitiza kuwa uhusiano uliopo kati ya Tanzania na China pamoja na jitihada za Tanzania kupitia TCAA ndio chachu ya utekelezwaji wa mradi huu ambao umefungua milango zaidi ya China kuisaidia Tanzania katika kuboresha miundombinu katika sekata ya Usafiri wa Anga.

Mkurugenzi Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Lucy Mbugua ameipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa kazi nzuri ambayo imefanya mpaka kuwa miongoni mwa nchi chache ambazo zimepata fursa ya mradi huu.

“Ni imani yangu kuwa kwa jitihada za serikali katika kukuza sekta hii mradi huu umetekelezwa mahali na wakati sahihi sana” alisisitiza Bi. Lucy

Akitoa maelezo ya awali, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari amesema tangu mradi huu ulipozinduliwa rasmi tarehe Januari 14, 2022 yapo mabadiliko makubwa na sekta ya usafiri wa anga imepiga hatua.

“Utekelezaji wa mradi huu umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95 na tayari tumeanza kuona matunda yake, Kama Taifa tunathamini sana jitihada zinazofanywa na ICAO katika kukuza na kuimarisha sekta hii muhimu kwa uchumi na usalama wa taifa letu na tutaendelea kufuata miongozo inayowekwa katika kuhakikisha anga la Tanzania linaendelea kuwa salama zaidi” alisema Bw. Johari.

Kikao kazi hicho kinachohudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo wa Usafiri wa Anga ndani na nje ya Nchi kitafanyika kwa muda wa siku 5 kuanzia Oktoba 30.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ally S. Possi akizungumza pamoja na kutoa shukrani kwa   Shirika la Anga Duniani (ICAO) kwa kukamilisha mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga ambao uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China uliogharimu takriban Dola Milioni Moja katika kikao kazi cha kuhitimisha mradi huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian akizungumza kuhusu Serikali ya  Jamhuri ya Watu wa China inavyoendelea kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kukamilisha mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga ambao uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China uliogharimu takriban Dola Milioni Moja katika kikao kazi cha kuhitimisha mradi huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari akizungumza kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyoweza kusamamia mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga ambao uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China wakati wa kikao kazi cha kuhitimisha mradi huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Lucy Mbugua akitoa pongeza kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa kazi nzuri ambayo imefanya mpaka kuwa miongoni mwa nchi chache ambazo zimepata fursa ya mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga ambao uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ally S. Possi aliyemwakilisha Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika kikao kazi cha kuhitimisha mradi huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ally S. Possi (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha za pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga kikao kazi cha kuhitimisha mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga ambao uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad