HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 4, 2023

TAASISI ya Mkapa Foundation Kuendelea Kutoa Mapendekezo Juu ya Upatikanaji wa Bima ya Afya

 TAASISI ya Mkapa Foundation imesema wataendelea kutoa mapendekezo yao kuhusu upatikanaji wa bima ya afya kwa wote ikiwemo watoto walio nje ya mfumo wa elimu.


Mkurugenzi anayesimamia mikakati na miradi wa taasisi hiyo, Dk Mussa Ndile akizungumza na Michuzi Tv, Michuzi Blog leo Oktoba 4,  2023, wakati wa mkutano wa kumi wa wadau wa Afya Tanzania ( THS)  unaoendelea kufanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(JINCC) jijini Dar es Salaam. Amesema Awanatambua kuwa serikali imesitisha bima ya afya ya watoto na kutokana na miongozo iliyotolewa hupata matibabu kwa vifurushi vya wazazi wao au shuleni.

Amesema wanaamini kupitia ushauri uliotolewa na wadau ikiwemo taasisi hiyo, mchakato wa bima ya afya kwa wote utakamilika.

Dk Ndile amesema taasisi yao inalenga kuwafikia  watanzania wasiofikiwa na huduma za afya katika maeneo magumu kufikika na kushauri kuhusu upatikanaji wa huduma za afya.

Amesema wamekuwa na mikakati ya kuimarisha mifumo ya afya ili kupata huduma bora  kwa kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali watu kwenye maeneo ya utoaji huduma ngazi za vituo vya afya na ngazi ya jamii.

Ameeleza kuwa wamekuwa wakihakikisha wanaimarisha mifumo na miongozo katika ukusanyaji mapato na wamekuwa wakihamasisha bima kwa wote ambayo ni nyenzo kubwa kufikisha huduma kwa watanzania.

" Tumekuwa na miradi mbalimbali tangu tulivyoanza timefikisha miradi 36 na miradi 14 inaendelea katika rasilimali watu, uhamasishaji wa mifumo ya afya na upatikanaji wa huduma bora," 

Pia wamekuwa wakihakikisha usimamizi bora wa huduma hizo kwa kuwepo na mifumo imara.
Mkurugenzi anayesimamia mikakati na miradi wa Taasisi ya Mkapa Foundation Dkt. Musa  Ndile, akizungumza na Michuzi blog/Michuzi TV leo Oktoba 4,  2023, wakati wa mkutano wa kumi wa wadau wa Afya Tanzania ( THS)  unaoendelea kufanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(JINCC) jijini Dar es Salaam.

Msimamizi wa Programu wa Taasisi ya Mkapa Foundayoon, Mwajabu Mbaruku akizungumza na wadau wa Afya waliotembelea banda lao wakati wa  mkutano wa kumi wa wadau wa Afya Tanzania ( THS)  unaoendelea kufanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(JINCC) jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad