
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
CHUO cha Taifa cha usafirishaji (NIT) kimeishukuru serikali kwa ndege mbili ilizokabidhiwa jana na kimesema kipo katika hatua za mwisho za kuanza kutoa mafunzo ya Urubani kwa garama nafuu ya ya asilimia 50 ulilinganisha na vyuo vya nje.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaami na Profesa Zacharia Mganilwa, Mkuu wa chuo cha NIT wakati wa mapokezi ya ndege ya abiria ya ATCL aina ya Boeing 737-MAX9 pamoja na uzinduzi wa ndege mbili aina ya Cessna Skyhawk za mafunzo ya Urubani kwa chuo hicho cha NIT
Amesema, NIT itatoza USD 48,000 sawa na Sh. Milioni 120.4 ambayo ni sawa na nusu ya garama ya mafunzo ya urubani nje ya nchi ambayo yanagarimu USD 100,000 ambazo ni sawa na Sh. Milioni 200 hadi 300
Mpaka sasa mafunzo ya Urubani yanaonekana kuwa ni taaluma ya watoto wa matajiri tu, lakini je Tanzania kuna matajiri wangapi, ila pia serikali kutoendelea kutoa ufadhili wa mafunzo ya urabani na uhandisi kwa muda mrefu imekuwa pia ikipunguza wanafunzi kusomea fani ya Urubani. Amesema Prof. Mganilwa.
Amesema, kumekuwepo na uhaba wa wataalamu wa sekta ya anga wakiwemo marubani jambo linalopelekea serikali kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi.
"Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa, wenye leseni ya biashara Katika eneo la usafiri wa anga waliosajiliwa ni 551 ambapo kati yao wageni ni 352 sawa na asilimia 64 na wazawa ni asilimia 36.
Aidha uongozi wa NIT, wakufunzi na marubani wanafunzi wameaswa kuzitunza ndege hizo ili ziweze kudumu na kuendelea kufundishia marubani walio wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment