HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 4, 2023

Engender Health Kufanya Tafiti Juu ya 'Jinsi,' Kubaini Faida na Athari Katika Upatikanaji Huduma za Afya


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Engenderhealth Tanzania, Dkt. Moke Makoma, akizungumza na Michuzi blog/Michuzi TV leo Oktoba 4,  2023, wakati wa mkutano wa kumi wa wadau wa Afya Tanzania ( THS)  unaoendelea katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(JINCC) jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Engenderhealth Tanzania, Dkt. Moke Makoma, akizungumza na wadau wa afya waliotembelea banda lake, leo Oktoba 4,  2023, wakati wa mkutano wa kumi wa wadau wa Afya Tanzania ( THS)  unaoendelea katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(JINCC) jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Engender Health Tanzania, Dkt. Moke Makoma amesema wanafanya utafiti kuhusu jinsi (Me na Ke) ili kubaini faida na athari zake katika upatikanaji huduma za afya.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza Mwandishi wetu katika banda wakati wa mkutano wa kumi wa wadau wa Afya Tanzania ( THS) unaoendelea kufanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(JINCC) jijini Dar es Salaam. Amesema kumekuwa na changamoto zinazotokana na jinsia ambazo zinahitaji kutatuliwa ili kuwa na huduma jumuishi za afya.

"Kuna changamoto baadhi ya wanawake hawawezi kufuata huduma za afya bila idhini ya mwenzi wake lakini pia wapo wanaume kufata huduma hizo wamekuwa wazito wanasubiri hadi kuugua," amesema Dk Makoma.

Amesema baada ya utafiti huo, watahakikisha kwamba dunia inakuwa ya usawa kwa jinsia zote na kwamba watatumia jukwaa hilo, kueleza kazi walizofanya Mkoa wa Tabora katika upatikanaji wa huduma hizo.

Dk Makoma amesema wana kongamano ambalo linahusiana na upatikanaji wa huduma jumuishi katika afya msingi kwa muktadha wa huduma za afya kwa wote.

"Tutaelwza ni namna gani kama nchi itafanya ili huduma hizo zipatikane kwa watu wote kuanzia zahanati, vituo vya afya na hospitali za Wilaya kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa na watanzania wenye afya njema na kutumikia taifa kwa uimara," amesema Dk Makoma.

Amesisitiza kuwa asilimia zaidi ya moja ya walemavu wamekuwa na muitikio kupata huduma za mkoba kutokana na kuwapatia elimu watoa huduma hizo.

"Tunafanya kazi katika Mikoa nane ya Tanzania Bara na yote ya Visiwani. Tupo Dar es Salaam, Pwani, Dodoma, Morogoro, Geita, Arusha, Kilimanjaro na Tanga," amesisitiza.

Pia amesema wana mada sita ikiwemo huduma za afya ya uzazi shirikishi kwa walemavu na vijana wamekuwa wakikabiliwa na changamoto pale wanapohitaji huduma ambazo watazitoa kwa wadau wa afya.

Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha mtu anapokwenda kupata huduma ya afya ya uzazi, apate na huduma nyingine zote kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad