HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 15, 2023

PROF.MKENDA: WAKUU WA WILAYA SIMAMIENI ELIMU YA WATU WAZIMA

Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda aakiwa katika banda moja wapo leo Oktoba 13 ,2023 katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kitaifa stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani. 

Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza leo Oktoba 13 ,2023 katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kitaifa stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Mkuu wa Wilaya ya Pwani, Abubakar Kunenge wakitembelea Mabanda leo Oktoba 13 ,2023 katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kitaifa stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Pwani, Abubakar akizungumza leo Oktoba 13 ,2023 katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kitaifa stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi na wanafunzi waliohudhulia katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kitaifa stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.


Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
WAZIRI wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia kwa weledi mpango wa utoaji wa elimu kwa watu wazima kwa sababu wao ndiyo Wenyeviti katika Wilaya zao.

Prof. Mkenda amesema kuwa Wakuu hao wa Wilaya wanatakiwa kuhakikisha elimu ya watu wazima inatolewa ikiwa hai na yenye uthibiti ubora.

Prof. Mkenda amesema hayo Oktoba 13 ,2023 ikiwa ni katika kilele cha maadhimisho hayo ya kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kitaifa stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani .

Aidha Prof. mkenda amewapongeza kutokana na kufana kwa kilele cha maadhimisho hayo huku amewataka waandaaji kuwa kupeleka sherehe hizo Mkoani Katavi ifikapo 2024 kwa sababu italeta chachu kwa Mikoa ambayo haina shughuli nyingi na kuweza kuketa hamasa zaidi kwa Wazee kupenda kusoma.

"Nawapongeza sana Mkoa wa Pwani kwa kuwa wenyeji katika kilele cha maadhimisho haya yamependeza na ari ya kusoma imeonekana hasa nikiangalia kundi la wazee waliojitokeza kwenye viwanja hivi"amesema Prof. Mkenda.

Viongozi wengine waliohudhuria kilele cha maadhimisho hayo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI),

Dkt.Charles Msonde ,Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof.Carolyne Nombo,Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani.

Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na DVV International, UNESCO, UNICEF na kusimamiwa na Baraza la usimamizi la TEWW.

Kauli mbiu yao imesema kuwa Kukuza Uwezo wa Kusoma na Kuandika kwa Ulimwengu Unaobadilika Kujenga Misingi ya Jamii Endelevu na nyenye Amani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad