HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 15, 2023

Washiriki wa SHIMIWI watoa Mil. 13.7 kusaidia wahitaji Iringa

 

Na Mwandishi Wetu, Iringa


WASHIRIKI zaidi ya 2800 wanaoshiriki kwenye michezo ya 37 ya Shirikisho la michezo ya Wizar ana Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), wamechangia kiasi cha shilingi milioni 13.7 za kununua mahitaji mbalimbali ya vituo vya wenye uhitaji vya mkoani Iringa.

Mratibu wa shughuli za kijamii wa SHIMIWI, Itika Mwankenja amesema kuwa fedha hizo zimetumika kununua vyakula vya aina mbalimbali, sabuni za unga na za mche, mafuta ya kula, mafuta ya kujipaka, maziwa ya Watoto wadogo, nguo za ndani za kike na kiume za Watoto, dawa za meno, miswaki, chumvi, sukari, madaftari, kalamu za wino, penseli, biskuti, pipi, kandambili aina ya yeboyebo, na nepi za kisasa za Watoto wadogo, pia wametoa fedha taslim kuanzia Tshs. Laki nane pamoja na uniti za umeme kwa vituo vinavyotumia umeme wa TANESCO.

Mwankenja amesema SHIMIWI inautaratibu wa kutenga siku moja wakati wa michezo kwenye mkoa inapofanyikia michezo hiyo na kupata fursa ya kutembelea wahitaji na kutoa msaada wa mahitaji muhimu baada ya watumishi wanaoshiriki kuchangishana wenyewe kwa wenyewe na kununua mahitaji hayo.

“Tunawashukuru sana watumishi kwa majitoleo yao kwani tumefanikisha lengo letu kwani mwaka ana hatukuiweza kufikisha milioni 10 lakini mwaka huu tumefikisha milioni 13, na tumeweza kutembelea vituo vinne vyenye watoto wenye na wazee wenye uhitaji vya Faraja House kilichopo eneo la Mgongo, Nyumbani Kwetu kipo Ismani, Huruma cha Tosamaganga na Amani cha Kitwilu, ambapo kote tumepeleka mahitaji hayo ambayo tunaamini yatawasaidia,” amesema Itika.

Amesema kwa upande mwingine watumishi wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, ambayo ndio wanahusika Zaidi na wenye uhitaji,kuwasaidia wenye uhitaji mbalimbali.

Hatahivyo, ametoa wito kwa Watanzania wote kujitokeza kuwasaidia wahitaji kwa chochote walichojaliwa, maana bado vituo vinauhitaji mkubwa wa mahitaji muhimu ya kijamii.

Naye Katibu Mkuu wa SHIMIWI, Alex Temba amesema kutokana na upendo mkubwa unaooneshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa watumishi, hivyo nao wanapaswa kuonesha upendo kwa wenye uhitaji.

“Hawa wenye uhitaji wanatutegemea sisi angalia katika vituo tulivyotembelea tumekuta vingine vinawatoto wa kuanzia mwezi mmoja, miaka miwili, mitatu hadi 22, ambao wote wanategemea misaada kwa sisi ambao tunauwezo,”amesema Temba.

Wakitoa shukrani kwa nyakati tofauti kwa msaada waliopewa Mtawa Helena Kigwele, msimamizi wa kituo cha Huruma kilichopo maeneo ya Tosamaganga amesema wamekuwa wakitegemea msaada kutoka kwa watu mbalimbali kutoka katika jamii.

Naye Padri Franco Sordella wa shirika la Consolata wa Faraja House iliyopo Mgongo amesema kituo chake kinapokea Watoto kutoka ofisi ya Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa, lakini hawana mahitaji muhimu Zaidi ya kutegemea kutoka kwa wasaria wema .

Michezo hii ya 37 ya SHIMIWI inatarajia kufungwa leo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro.Mmoja wa waratibu wa zoezi la kurudisha kwa jamii yenye uhitaji wa mkoa wa Iringa, Gabriel Samson, ambaye pia ni meneja wa t imu ya Uchukuzi (kushoto) akimkabidhi fedha za kununua mahitaji madogo madogo msimamizi wa kituo cha Nyumbani Kwetu, Bw. Felix kilichopo Ismani mkoani Iringa.Watoto wenye uhitaji wanaoishi katika nyumba ya Faraja iliyopo eneo la Mgongo mkoani Iringa wakionesha madaftari waliyogaiwa ikiwa ni baadhi ya vitu muhimu walivyopewa na washiriki Zaidi ya 2800 wa michezo ya 37 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), inayofanyika mkoani Iringa.Mratibu wa Shughuli za Kijamii wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), Itika Mwankenja (kushoto), akimkabidhi Mtawa Helena KigweleMakamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzaia (SHIMIWI), Michael Masubo (kushoto) akiwapa madaftari wanafunzi wanaoishi kwenye nyumba ya wenye uhitaji ya Amani iliyopo iwiru mkoani Iringa, ikiwa ni desturi ya washiriki kwa michezo ya SHIMIWI ya kurudisha kwa jamii katika kituo cha mashindano.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad