HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 26, 2023

OKTOBA 29 TCAA KUADHIMISHA MIAKA 20 KWA MBIO ZA HISANI

 

Mwenyekiti wa Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA Mellania Kaseke katikati,  Isaya Mwakifulefule Meneja Mawasiliano  na Uhusiano wa Taasisi wa TCAA na  kushoto ni katibu wa Chama Cha Riadha  mkoa wa Dar es salaam, Samweli Mwela, wakionyesha vifaa vitakavyotumika katika mbio za hisani za kilometa tano na kilometa 10 ikiwa katika kuadhimisha miaka 20 ya TCAA
Mwenyekiti wa Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA Mellania Kaseke katikati,  Isaya Mwakifulefule Meneja Mawasiliano  na Uhusiano wa Taasisi wa TCAA n  kushoto ni katibu wa Chama Cha Riadha  mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela, wakionyesha vifaa vitakavyotumika katika mbio za hisani za kilometa tano na kilometa10 ikiwa katika kuadhimisha miaka 20 ya TCAA
Mwenyekiti wa Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA Mellania Kaseke akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 26, 2023 jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi ya mbio hizo za hisani zinazotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2023 katika viwanja vya Mlimani City pamoja na siku ya  mjadala wa wadau wa sekta ya Anga Oktoba 30, ikiwa ni kuadhimisha miaka 20 ya TCAA, kulia ni Isaya Mwakifulefule Meneja Mawasiliano  na Uhusiano wa Taasisi wa TCAA na  kushoto Kwake ni katibu wa Chama Cha Riadha  mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela.
katibu wa Chama Cha Riadha  mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela. Kushoto akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 26, 2023 jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi ya mbio hizo za hisani zinazotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2023 katika viwanja vya Mlimani City ikiwa ni kuadhimisha miaka 20 ya TCAA kulia kwake ni , Mwenyekiti wa Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA Mellania Kaseke.


Na Karama Kenyunko Michuzi tv

KATIKA kuadhimiasha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA) nchini, Mamlaka hiyo imeandaa  mbio za hisani za Km tano na km 10 sambamba na mjadala wa wadau wa sekta ya Anga ili kujadili mafanikio na changamoto katika sekta hiyo.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Oktoba 29 katika viwanja vya Mlimani City ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila akitarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mbio hizo huku Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Kassim Majaliwa akitarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mjadala wa wadau wa sekta ya Anga. 

Mwenyekiti wa Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA Mellania Kaseke amesema hayo leo Oktoba 26, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam juu ya maandalizi ya mbio hizo pamoja na mjadala wa sekta ya Anga.

Akizungumzia mbio hizo za hisani  Kaseke amesema  mpaka sasa teyari maandalizi ya mbio hizo yamekwisha kamilika ambapo zitakuwa za Km 5 hadi Km 10 huku pia wafadhili mbali mbali wakiwa wamejitokeza kufadhili mbio hizo ili kuhakikisha maazimisho hayo ya miaka 20 ya TCAA yanafana. 

"Ninawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kushiriki na wale watakaokosa nafasi basi wasisite kuja kuangalia, tutaanza na mbio za KM 5 hadi KM 10, vifaa vyote vimeishawasili na mbio zitaanza saa 12.00 alfajiri siku hiyo ya Oktoba 29, 2023" amesema Kaseke.

"Shamra shamra za  Maadhimisho haya zimekuwa zikiendelea  yakiendelea lengo likiwa kuzungumzia mafanikio yaliopatikana katika miaka hiyo 20 mpaka sasa maandalizi yamekamilika vifaa vyote vimeishawasili na Octoba 30 kutakuwa na mjadala wa wasafiri wa Anga , ameongeza Kaseke

Aidha amesema lengo ni kuu la mbio hizo ni kuunga  mkono  jamii iliyoko katika maeneo ya ukame iweze kupanda miti ya kutosha Ili kupunguza uhalibifu wa hali ya hewa.

Akizungumzia kuhusiana na siku ya mjadala wa wadau wa sekta ya Anga, Kaseke amesema, lengo kubwa ni kuwakutanisha pamoja  na kujadili mafanikio na chagamoto mbalimbali zilizopo katika tangu kuanzishwa kwake.

Mjadala huo utatoa nafasi kwa wadau wa sekta ya usafiri wa Anga kutoa chagamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kutimiza wajibu wao.

"Oktoba 5 mwaka huu Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka hii alizindua Maadhimisho haya na kuweka  bayana  mafanikio na chagamoto katika miaka 20 ya Maadhimisho haya hivyo hii ni Moja ya njia ya kukutana na wadau wa sekta hii kujadiliana mambo mbalimbali."

Kwa upande wake, katibu wa Chama Cha Riadha  mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela amesema  wamekuwa wakishirikiana na TCAA katika maandalizi ya mbio hizo kwa kuwa chama hicho ndio kimekuwa kikihusika katika mbio zote hapa 

"Tumeshirikiana kwa maandalizi yote, njia watakazopita zimepimwa na ziko katika hali ya usalama, na tunaamini michezo ni sehemu ambayo inapeleka ujumbe kwa wepesi sana, na kwa watu wengi na wakati mmoja", amesema Mwela 

Changamoto kwa watu wengine  kutohusisha chama cha riadha jambo ambali linahatari sana kwa sababu likitokea 

Aidha ametoa wito kwa wadau wengine wanaofanya mbio kama hizo bila ya kuhusisha chama cha riadha kuacha kufanya hivyo kwani ikitokea jambo ambalo siyo la kawaida hautakuwa na mahali pa kusema wala kusimama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad