HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 20, 2023

BINGWA WA MASOMO YA HISABATI ATANGAZWAChama Cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) kimetoa orodha ya wanafunzi 233 kati ya 812 waliofanya vizuri katika shindano la hisababti Nchini Tanzania.

Wanafunzi hao kutoka mikoa 11 ya Tanzania bara na visiwani, walipata asilimia 40 na zaidi ya alama zilizohitajika kwenye shindano hilo na wengine 579 wakipata chini ya asilimia 40.

Mtihani huo ulihusisha makundi mawili, kundi la kwanza likiwa ni wanafunzi wa kidato cha tatu hadi cha nne na kundi la pili ni kidato cha tano hadi sita na washindi.

washindi hao wanatoa wanatoa mwanya wa kupatikana kwa washiriki nane katika shindano la hisabati ngazi ya Afrika mashariki, Afrika na Dunia litakalofamyika mapema mwakani

Akisoma matokeo hayo jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHAHITA Betinasia Manyama,alitaja badhi ya wanafunzi wa kundi la wanafunzi 10 bora wa jumla kidato cha tatu na nne akiwemo Stella Maliti wa Shule Marian Girls ya Pwani, Brown Mafuru wa Marian Boys Pwani na Alice Gonza wa Canossa ya Dar es Salaam.

Kuhusu ya idadi ya shule zilizoshirikia, alisema ni 58 wanafunzi wakiwa 540 ambapo waliopata asilimia 40 na kuendelea ni 167 na chini wastani huo ni 373.

Kwa kidato cha tano na sita, Betinasia alisema walioshiriki ni 272 kutoka shule za sekondari 22, wavulana wakiwa 162 na wasichana 110 takwimu zikionyesha waliopata asilimia 40 na zaidi ni 66 pekee na wenye upungufu na wastani huo wakiwa 206.

Baadhi walioshika nafasi 10 za mwanzo ni Amosi Paulo wa Mzumbe mkoani Morogoro,Elia Wambura wa Iyunga Technical Mbeya na Mwanaarab Said wa Lumumba mjini Magharibi.

Betinasia alisema mtihani wa kuwapata washindi ulifanyika Agosti mwaka huu na washindi nane wanasakwa kuiwakilishi nchi kwenye mashindano ya hisabati Afrika Mashariki, Afrika na Duniani.

“Lengo la mashindano haya ni kupata wanafunzi watakaoiwakilisha nchi kushiriki katika mashindano ya kimataifa,pia kujenga ushirikiano wa kitaaluma na mataifa mbalimbali duniani,baada ya matokeo haya washidi 10 kwa kila jundi watapatiwa zawadi siku ya maadhimisho ya Hisabati Duniani Machi14,2024”alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHAHITA Dk Said Sima alisema malengon yao mwakani ni kuhakikisha mikoa yote nchini inashiriki shindano hilo.

Alisema si kila mwanafunzi anashiriki bali ni wale wenye vipaji na uongozi kwenye shule husika ndio huwachagua wahusika kuingia kwenye shindano hilo la mitihani ya hisabati.

“Tunaweka mikakati hawa washindi tuwape elimu ya kutosha ili washiriki kwenye mashindano ya kimataifa vyema,”alisema.

Naye Mkuu wa Idara ya Hisabati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Sylvester Rugeihyamu alisema lengo la shindano la hisabati ni kutambua na kuibua vipaji kwenye somo hilo,kuchochea na kutambua ubunifu wa uvumbuzi kupitia mitihani

Pia kuwapa motisha wanafunzi kuipenda somo la hisabati akisistiza mitihani hiyo haitumii mitaala inayotumiwa na Baraza l;a Mitihani Tanzania (Necta)

Mikoa ambayo imetoa shule zilizoshiriki kwenye shindano hilo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Mbeya,Arusha,Dodoma, Iringa,Kilimanjaro, Songwe,Mwanza na mjini Magharibi.
Mwenyekiti wa Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA), Betinasia Manyama, akitangaza matokeo ya mitihani ya mashindano ya hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, nne, tano na sita, katika Idara ya Hisabati, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Said Sima na kulia ni Mkuu wa Idara ya Hisabati na Mlezi wa CHAHITA, Dk. Sylvester Rugeihyamu. na mpiga picha wetu

Katibu mkuu wa chama cha hisabat Said Sima mara baada ya kutangazwa matokeo ya mitihani ya mashindano ya hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, nne, tano na sita, katika Idara ya Hisabati, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana,kulia ni Mkuu wa Idara ya Hisabati na Mlezi wa CHAHITA, Dk. Sylvester Rugeihyamu.

Mkuu wa Idara ya Hisabati na Mlezi wa CHAHITA, Dk. Sylvester Rugeihyamu akizungumza jambo mara baada ya kutangazwa matokeo ya mitihani ya mashindano ya hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, nne, tano na sita, katika Idara ya Hisabati, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana,

Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad