HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 20, 2023

Y9 Microfinance yakabidhi mshindi wa pikipiki, washindi wawili wapatikana wa droo ya mikopo ya aina tatu


Na Mwandishi wetu.


Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance imemzawadia George Kivuyo pikipiki baada ya kuibuka mshindi wa droo ya kwanza ya wateja wao inayowawezesha kupata huduma tatu tofauti za mikopo.

Kivuyo alikabidhiwa na Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya katika halfa fupi iliyofanyika jana na kumpongeza mshindi huyo kwa kujiunga na huduma zao.

Mbali ya Kivuyo, droo ya kwanza pia ilimpata mshindi wa simu ya mkononi ambapo Ummukulthum mkazi wa Zanzibar.

Mang’enya alisema kuwa Kivuyo ameshinda zawadi hiyo baada ya kukopa kupitia app yao na baadaya kutumia mikopo hiyo, walirejesha mikopo hiyo ndani ya siku tatu kwa mujibu wa taratibu.

Alifafanua kuwa wateja wao wanaweza kukopa fedha taslimu, fedha ya malipo ya umeme (LUKU) na muda wa maongezi kwa kutumia ‘app’ yao ambayo lazima uipakue (download).

“Zawadi zpo bado nyingi kwani tutakuwa na droo ya kila wiki na kuwazawadia washindi wawili. Mshindi wa pikipiki na simu janja ya mkononi. Hii ni fursa kwa wateja wetu,” alisema Mang’enya.

Kwa upande wake, Kivuyo alisema kuwa hakuamini kama ameshinda na ataitumia pikipiki hiyo katika biashara zake ndogodogo.

“Nimefurahi sana, nilikopa kiasi kidogo sana cha fedha na baada ya kutumiza mahitaji yangu, nilirejesha. Kiasi kidogo cha mkopo huo, kimeniwezesha kupata zaidi kubwa kabisa, hii ni historia kwangu,” alisema Kivuyo.

Wakati huo huo, taasisi hiyo imewapata washindi wa droo ya pili ya pakua app ya Y9 ili uweze kupata huduma tatu za mikopo.

Katika droo hiyo, Anni Chimenya ameshinda pikipiki huku Jaqueline Jumla akishinda simu ya mkononi. Washindi hao watazwadiwa zawadi zao katika droo ya wiki ijayo.

Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini,Salim Bugufi aliipongeza washindi hao na kuwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo ili kufikia malengo yao.

Meneja Masoko wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Sophia Mang’enya akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa droo ya pili taasisi hiyo. Kampeni hiyo pia itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya Samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST. Kulia ni Msimamizi kutoka michezo ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Salim Magufi na kushoto ni mshindi wa pikipiki wa droo ya kwanza George Kivuyo.
Meneja Masoko wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Sophia Mang’enya (kulia) akimkabidhi mshindi wa pikipiki wa droo ya kwanza taasisi hiyo George Kivuyo. Kampeni hiyo pia itamwezesha wateja wao kushinda pia simu ya mkononi .

Msimamizi kutoka michezo ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Salim Magufi akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa droo ya pili ya taasisi hiyo Y9 Microfinance. Taasisi ya Y9 Microfinance kwa sasa inaendesha kampeni ambayo itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya Samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST.


Mshindi wa droo ya kwanza ya Y9, George Kivuyo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki. Taasisi ya Y9 Microfinance kwa sasa inaendesha kampeni ambayo itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya Samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad