HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 29, 2023

DC MATINYI AWATAKA WAKAZI WA TEMEKE KUBADILISHA MTAZAMO KUHUSU USAFI

 

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi (katikati) akipanda mti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira, alipoongoza zoezi hilo leo Septemba Septemba 29,2023.

Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi leo Septemba 29 2023 ameongoza zoezi la upandaji miti 500 katika Kata ya Buza kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na wadau wa Mazingira pamoja na wananchi.

Mhe. Matinyi ametoa wito kwa wakazi wa Temeke kubadilisha mtazamo juu ya suala zima la mazingira hasa kuweka msisitizo upandaji wa miti.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi Bayport Yeriko Mtemvu amesema kuwa wameamua kurudisha kwa jamii kwa kupanda miti 500 katika Kata ya Buza ili kushiriki vyema utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Tunashukuru kuungana na Viongozi wa Wilaya ya Temeke kushiriki kupanda miti katika kurudisha kwa jamii ili kwa pamoja tutunze mazingira, tutapanda miti 500 na tutaitunza kwa siku 60 lengo kubwa miti hii istawi ili itunze mazingira yetu na kuleta hewa safi" amesema Mtemvu.

Aidha Wilaya ya Temeke inaendelea na usafishaji wa mazingira hususani katika mitaro ili kujiandaa na mvua za El Nino zinazotarajiwa kuanza kunyesha hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad