Kesi ya Mauaji ya Dada wa Bilionea Msuya Yaendelea Kuunguruma Mahakama Kuu - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 21, 2023

Kesi ya Mauaji ya Dada wa Bilionea Msuya Yaendelea Kuunguruma Mahakama Kuu

  SHAHIDI wa 18 katika kesi ya Mauaji inayowakabili aliyekuwa mke wa Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake ameieleza mahakama kuwa aliyemtambua mshtakiwa wakati wa gwaride la utambuzi akisikia akisema kuwa Miriam allimshikia  bastola.

Shahidi Sophia Amir Shemzigo(46) na mama ntilie ambaye kwa sasa anaishi Songea, ameeleza hayo leo Agosti 21,2023 wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Edwin Kakolaki wa mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.


Washtakiwa katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 ni wifi wa marehemu, Aneth, mjane wa Bilionea Msuya; Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella.

Aneth alifariki dunia Kwa kuchinjwa shingoni Mei 25, 2016, usiku nyumbani kwake, Kibada Kigamboni, wilayani Temeke (wakati huo).


Akiongozwa na wakili wa serikali Generosa Montana,  Sophia ambaye zamani alikuwa akishi Dar es Salaam eneo la kurasini amedai kuwa, Agosti 7, 2023 akitokea kudai madeni yake ya chakula eneo la Jkt Mgulani aliitwa na askari polisi wa kituo cha Kilwa road akimtaka ashiriki Gwaride la utambuzi.

Amedai alikubali ndipo askari huyo atamchukua hadi nyuma ya kuituo hicho cha polisi ambapo alikutwa wanawake wengine saba na yeye akawa wa nane.

"Tulipangwa mstari na msimamizi wa gwaride ambaye alikuwa ni askari wa kiume akatuambia kuna utambulisho na kwamba kuna mtuhumiwa wa mauaji anatakiwa kutambuliwa. Ndipo wakati wamesimama pale mtuhumiwa alipelekwa n kusimama pembeni yake.

Amedai kuwa baada ya kuwa wamejipanga mstari askari mmoja wa kike alimpeleka msichana is  na kumwambia apite kwenye gwaride lile kwa nyuma na mbele

"Wakati anapita alipofika kwa mbele alimshika bega la kushoto mtuhumiwa akatamka 'Huyu ndio ambae alikuja nyumbani kwa tajiri yangu Kigamboni akanitishia kwa bastola kuwa ondoka'

Amedai baada ya hapo mtuhumiwa alichukiliwa na askari wa kike akaondoka nae na sisi tukapewa karatasi tukasiani na kuruhusiwa kuondoka.
baada ya kumaliza kuto ushahidi wake, wakili wa utetezi Peter Kibatala alimuhoji mshtakiwa ambapo mahojiano yao yalikuwa:


Kibatala: Shahidi wakati unaongozwa na wakili hapo kutoa ushahidi, ulimwambia Jaji kwamba kwenye hii karatasi kuna namba zako za simu walizotumia kukuita?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba Ulitoa namba zako za simu wakikuhitaji wakupate?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unajua Kiingereza

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba kabla ya kujaza hii fomu Afisa yule alikufafanulia kilichomo?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Kwa hiyo hata nikikuonesha hii kwamba hapa wameandika eight, wakasaini hujui?

Shahidi: Mimi sijui Kiingereza

Kibatala: Katika karatasi hii ni wapi Jaji na w wakisoma kuna majina ya Sophia Amir Shemzigo?

Shahidi: Sophia Amir

Kibatala: Kuna Shemzigo?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Wakati unatambulishwa ulimwambia Jaji kuwa hapa naona Sophia Amir lakini ni mtu mmoja?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Shahidi wewe si Mwanasheria wala Polisi lakini kuna masharti ya lazima.Ulimwambia Jaji kuwa wakati wa utambuzi huyu mtuhumiwa hakuwa na pingu?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Jaji kuwa yule mama aliyetambuliwa alikuwa hana alama yoyote, hajavimba au kuchubuka usoni?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba wewe huna uhusiano wowote na afisa wa Polisi?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba wewe hauna huba husuda na wala chuki na huyu dada?

Shahidi: Sijamwambia


Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba wewe ulikuwa huna wala humfahamu huyu mshtakiwa wala ndugu wa marehemu?

Shahidi: SijamwambiaKibatala:  Shahidi, hii kesi umekuwa reported kwenye vyombo vya habari je ulimwambiaJaji kwamba utambuzi wangu hauhusiani na kuona picha yake kwenye magazeti?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Shahidi ulimwambia Jaji wale maafisa wa Ukaguzi walimpa nafasi mtuhumiwa kumkataa yeyote pale?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala:  Shahidi umesema tu binti aliyekuja alisema maneno...

Shahidi: Ehee

Kibatala: Mwambie Jaji kama ulimsikia.aiitaja tarehe na mwaka

Shahidi: Hakutaja tarehe

Kibatala: Ulimsikia huyo dada akisema hata hivyo namfahamu niliwahi kumuona Mererani kwa mama Aneth 

Shahidi: sijamsikia


Kesi hiyo inaendelea kesho kwa shahidi wa 19 wa upande wa Jamuhuri kutoa ushahidi wake.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad