HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 21, 2023

PAPI KOCHA ,ELOMBE KICHINJA WAHAMIA TOWN CLASSIC BENDI

 Na Khadija Seif, Michuziblog
MWANAMUZIKI wa dansi nchini, Jonhson Nguza ‘Papii Kocha’ amesajiliwa na kutambulishwa kama Muimbaji wa bendi ya Town Classic kwa lengo la kuongeza nguvu katika bendi hiyo.

Mbali na Papii Kocha bendi hiyo imesajili wanamuziki wengine ambao ni Amri Francis na Fayed Basizi pamoja na Mpigaji wa solo Elombe Kichinja.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Pactrick Kessy amesema usajili huo utaleta tija katika kukuza tasnia ya muziki na bendi yao kiujumla.


“Tumemsajili Papii Kocha na wenzake kwa lengo la kuja kupambana na kuongeza nguvu katika bendi yetu, pia kurudisha hadhi ya muziki wa dansi."

Patrick amewata mashabiki wa bendi hiyo wategemee kuona mambo mazuri kutoka kwao, pia nyimbo zenye ushindani zikitungwa.

Mwanamuziki, Papii Kocha amesema mashabiki wa muziki wa dansi na wategemee nyimbo zenye maudhui mazuri kutoka kwake.

“Nitahakikisha hadi ikifika miezi sita nitakuwa nimetunga nyimbo ambazo zitakuwa katika mfumo wa ablamu ambazo zitaleta ushindani katika tasnia ya muziki nchini."

Papii Kocha amabye alitamba na ngoma ya ‘Seya’ ilifanya vema hapo awali alikuwa katika bendi ya Tukuyu Sound akishirikiana na Kalala Junior.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad