COREFA WAZINDUA KITUO CHA MICHEZO CHINI YA UMRI WA 14,17 NA 21 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 21, 2023

COREFA WAZINDUA KITUO CHA MICHEZO CHINI YA UMRI WA 14,17 NA 21

 Na Khadija Kalili Michuzi Tv

MWENYEKITI wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) Robert Munisi amesema kuwa amefurahishwa kutimiza ndoto ya kuzindua Kituo cha kufundisha soka kwa watoto wenye umri wa miaka 14, 17 na 20 ambacho kitakua kikitoa mafunzo hayo mara mbili kwa juma.

Munisi amesema hayo leo Agosti 20 kwenye uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Bwawani , Mailimoja Kibaha na kuhudhuriwa na watoto wengi ambao walifika katika uzinduzi huo.

"Hii ilikua ni njozi yangu na kwa mara ya kwanza COREFA imeandika historia kwa kuanzisha mpango huu wa kuwafundisha watoto wa chini ya umri wa miaka 14,17 na 20 soka na kuibua vipaji hapo baadaye tunatarajia kuwaleta wataalamu kutoka katika 'Academy' mbalimbali ili waweze kuwachukua na kuendeleza vipaji vyao "amesema Munisi.

Amesema kuwa mpango huu wa kuwa na vituo utafanyika ndani ya Mkoa wa Pwani huku kila Wilaya inatakiwa kuwa na vituo vitatu,baada ya Kibaha watakwenda kuzindua Mlandizi na Chalinze.

Baadaye watakwenda Bagamoyo, Kibiti, Mkuranga, Rufiji Kisarawe na Mafia.

Munisi amesema kuwa mbali ya kuwafundisha vijana soka pia watafundishwa masuala ya uamuzi na ukocha ambapo kwa wale watakaokuwa wamefanya vizuri watapewa kazi ya kuwa waamuzi na wachezeshaji kwenye michuano mbalimbali ya Kiwilaya na hata ngazi ya Mkoa.

"Tunawaomba wazazi wawalete watoto wao waje kujifunza soka kwa sababu michezo ni ajira wachangamkie fursa hii, amesema Munisi.

Katika kituo hicho kutakuwa na miundombinu rafiki ambayo itawawezesha kujifunza soka sanjari na madaktari watakuwepo endapo mtoto ataumia.

Katika uzinduzi huo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha Moses Magogwa alikua mgeni rasmi ambapoamemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon.

Magogwa amewapongeza COREFA kwa hatua hiyo na amewaaahidi kuzifanyia kazi changamoto ambazo zinawakabili ambazo ni ukosefu wa kiwanja cha michezo pamoja na Ofisi kwa Chama Cha Soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) na COREFA huku suala la Uwanja amesema kuwa amelichukua kama serikali ambapo atakwenda kuliwasilisha na kufanya mazungumzo na Halmashauri ili kuona namna ya kuwapa eneo ambalolitakua maalumu kwa kukuza vipaji ndani ya Mkoa wa Pwani.

" Mipango iko mingi tunalibeba jambo hili kama serikali ili vyana vyetu vya soma waweze kupata Kiwanja,Ofisi KIBAFA na COREFA hii ni baada ya kusikia changamoto waliyonayo" amesema Magogwa.

Mafunzo hayo yatakua yakifanyika mara mbili kwa wiki yaani Jumamosi na Jumapili pamoja na siku zingine zitakazokuwa za mapumziko.
Baadhi ya watoto wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Moses Magogwa kwenye uzinduzi wa Kituo hicho uliofanyika katika viwanja vya Bwawani
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Kibaha Moses Magogwa akimkabidhi mpira Mratibu wa Kanda ya Kaskazini Abubakari Alawi, anaye shuhudia katikati ni Mwenyekiti wa COREFA Robert Munisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad