UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO KATIKA MAONESHO YA SABASABA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 30, 2023

UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO KATIKA MAONESHO YA SABASABA

 

TAASISI  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kwamba inashiriki maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28/06/2023 hadi tarehe 13/07/2023.

Katika maonesho haya tunafanya upimaji na kutoa ushauri wa kiafya kuhusiana na magonjwa ya moyo, kuelezea kwa kina huduma zinazotolewa na Taasisi na kutoa matibabu ya hapohapo kwa wagonjwa wanaokutwa na matatizo ya moyo yanayohitaji kupewa rufaa.

Madaktari wetu mabingwa wa magonjwa ya moyo Tulizo Shem, Tatizo Waane, Delilah Kimambo, Honaratha Maucky, Baraka Ndelwa na Pedro Pallangyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Peter Kisenge wapo katika banda letu kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Wananchi wote mnakaribishwa kutembelea Banda letu lililopo ndani ya banda la Jakaya Kikwete ili muweze kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na afya ya moyo.Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ipo kwaajili ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya moyo.

“Afya Bora ya Moyo kwa Ustawi wa Biashara na Uwekezaji Tanzania”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad