SERIKALI IPO TEYARI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUKUZA UCHUMI WA KIDIJITALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 24, 2022

SERIKALI IPO TEYARI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUKUZA UCHUMI WA KIDIJITALI

SERIKALI ipo teyari kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ili kuhakikisha uchumi wa kidijitali unakua nchini. Katika Malengo ya maendeleo endelevu ya tano ya uchumi wa kidigitali umetengeneza fursa nyingi kwa watanzania katika teknolojia ya Mawasiliano.

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrew wakati akifungua mjadala wa 9 wa jukwaa la Utawala wa Mtandao Tanzania Novemba 23, 2022 jijini Dar es Salaam amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza katika miundombinu teknolojia ya mawasiliano ili kuwafikia watanzania wa Mjini na Vijijini.

Mhandisi Kundo amesema kuwa lazima watanzania wajengewe uwezo ili kufaidi matunda ya miundombinu hiyo ambayo serikali imewekeza kwani wao ndio watumiaji.

Na ili kuhakikisha teknolojia ya Mawasiliano inakua hapa nchini Mhandisi kundo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepewa maelekezo ya kujenga Chuo cha Masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano ambapo kitawezesha watu mbalimbali kujifunza.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa maelekezo kwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhakikisha chuo cha Masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano kinajengwa nchini." Amesema Mhandisi Kundo

Kwa Upande wa Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Dkt. Seleman Arthur amewaasa Watanzania wahakikisha wanajiandaa kwa mapokeo ya Sheria ya Makosa ya mtandao ambayo itatenda haki pale mtu anapofanya makosa Mtandaoni.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada kwa jukwaa la utawala wa kimtandao wa Intaneti, amesema kuwa kutokujua kosa sio kigezo cha mtu kutokushtakiwa pale atakapotenda kosa mtandaoni hivyo wananchinwajiandae kuwa raia wema mtandaoni.

Amesema kuwa sheria hiyo itawakamata hivyo kwa kuwa itawasumbua ni bora waachane na mawazo ya kufanya uhalifu mtandaoni

Kwa upande wa Rais wa Shirika la Internet Society Tanzania, Naza Nichorus amesema kuwa mkutano wa 9 wa jukwaa la Utawala wa Mtandao Tanzania unawezesha wadau mbalimbali kuchangia mada na kuzungumza nini kifanyike katika mtandao kwa maendeleo ya taifa.

Amesema kuwa majadiliano hayo yanalengo la kusimamia mtandao wa Intaneti hapa nchini kwa sababu mtandao huo haujawahi kuwa wa mtu mmoja, jamii kwa ujumla lazima kusimamia mtandao huo.

"Intaneti tangu ilipoanza imekuwa chombo ambacho kinafanyiwa kazi, kinaendeshwa, kinaboreshwa na wadau wote ndio maana kila mdau yupo hapa kujadili mada."Amesema Nichorus

Akizungumzia kuhusiana na makundi mbalimbali yenye mahitaji maalumu, Nichorus amesema katika mkutano huo kunawatu wasioona na intaneti inawasaidia kutokana na kuwa na program mbalimbali ambazo wanaweza kuzitumia ili kuweza kushiriki kwa kutumia 'Internet Accesibility ' ambayo inamifumo ambayo ni tofauti na watu ambao wanaona na kusikia.

Kwa upande wa wadau mbalimbali katika mkutano huo wameonesha kufurahishwa na wananchi kutumia vizuri mtandao wa intaneti kwa manufaa ya kujiingizia kipato.

Mmoja ya washiriki alijibu swali kwa njia ya mtandao, amesema kuwa ili kuhakikisha kila mtanzania anatumia interneti ipasavyo wamepanga kuweka intaneti ya jamii 'Pubic Internet' katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar Mzena Hospitali na katika eneo la Kiembe samaki Zanzibar ambapo kila mwananchi atakuwa na uwezo wa kutumia mtandao huo bila kulipia.

Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrew akizungumza wakati akifungua mjadala wa 9 wa jukwaa la Utawala wa Mtandao Tanzania Novemba 23, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Dkt. Seleman Arthur akizungumza wakati wa kuwasilisha mada kwa wadau wa Mkutano wa 9 wa  jukwaa la Utawala wa Mtandao wa Interneti nchini.
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania (NGOs) Neema Lugangira akizungumza akizungumza wakati wa mjadala wa 9 wa jukwaa la Utawala wa Mtandao Tanzania Novemba 23, 2022 jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wanajukwaa la Utawala wa Mtandao wa intaneti wakisikiliza watoa mada mbalimbali wakati wa kufunguliwa  kwa mjadala wa 9 wa jukwaa la Utawala wa Mtandao Tanzania Novemba 23, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mdahalo ukiendelea wa Masuala ya Mtandao wa Intaneti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad