HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 25, 2022

Chuo Cha Kodi Kinawajibu kutoa wataalam wenye umahili katika Masuala ya Forodha na Kodi- Mafuru

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence  Mafuru akimtunuki cheti mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo kwa ngazi ya Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM), Edwin Norasco wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaama leo Novemba 25, 2022. 

CHUO Cha Kodi Kinawajibu wa Kuhakikisha kwamba kinatoa wataalam wenye umahili katika Masuala ya Forodha na Kodi ambapo wataiwezesha serikali kukusanya mapato na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa Kodi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence  Mafuru akizungumza wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaama leo Novemba 25, 2022. Amesema kuwa Katika kufanyikisha malengo ya serikali Chuo kinatakiwa kufanya tafiti ambazo zitaleta majibu ya changamoto za Kikodi zinazoikumba taifa. 

Amesema katika Mpango wa miaka mitano ya Maendeleo serikali inalenga kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya Nchi na Maendeleo ya watu.

Amesema kuwa maendeleo hayo yanatakiwa kufikiwa kama kutakuwa na ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kidijitali.

"Ukuaji wa Mapato ya ndani ndio njia ya uhakika inayowezesha kujenga maendeleo ya nchi, kunawakati tulitegemea misaada na Mikopo kutoka nchi na taasisi mbalimbali lakini kunaukomo katika utegemezi huo njia pekee ni sisi wenyewe kusimamia shughuli zetu za kiuchumi na kuweka sera za kiuchumi pamoja na usimamizi na kuongeza mapato ya ndani ili tuweze kuwa na maamuzi ya kuumua na kutekeleza mipango yetu wenyewe." Amesema Mafuru.

Aidha Mafuru amewaasa wahitimu kutumia elimu waliyoipata katika kuleta majibu ya changamoto zilizopo na kuwa na mikakati ambayo itawezesha taifa kwenda mbele.

Amesema ni wakati mwafaka sasa kujipanga kuendana na mabadiliko ya kiuchumi hasa katika zama hizi za mapinduzi ya nne ya viwanda ambayo yanachagizwa na matumizi makubwa ya Teknolojia na mifumo ya kidijitali. 

Amesema walipa kodi wengi sasa wanahamia kulipa kodi kidijitali hivyo ni wakati mhimu kwa wahitimu hao kuwa vinara wakati wanajipanga kwa kuwa na utaalamu katika mifumo ya kiteknolojia ambayo inawawezesha kwenda kwa kasi ya mabadiliko yanayotokea  kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi. 

Amesema serikali bado haijapata mbinu bora ya kukusanya mapato ya shughuli za kiuchumi yanayopatikana kwenye biashara zianazoendeshwa mtandaoni, sababu moja wapo ni kutokuwa na wataalamu wa kutosha. 

"Niwaombe suala hili lipewe kipaumbele katika mitaala yenu ili tuweze kuwajengea uwezo watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wataalamu wengine wa kodi nchini, tunahitaji kuendana na kasi ya Mabadiliko haya nchini kwa kuwekeza katika ujuzi na Utaalamu pamoja na mifumo ya kisasa." Amesema Mafuru

Mafuru amesema kuwa wakati serikali inaendelea kuifungua nchi na kukaribisha wawekezaji kutoka nje. Nchi yetu inaingia sasa kuwa sehemu ya uchumi mpana wa dunia (Global Economy).

Amesema tunatakiwa kuendelea kuimarisha  wetu kwa kuwa na wataalamu katika kuangalia mifumo ya kodi kimataifa. 

Kwa Upande wa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Isaya Jailo amewaasa wahitimu kutumia vizuri elimu waliyoipata kwa manufaa yao na manufaa ya taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa wahitimu hao ni wanawake 198 na wanaume 291  wamemaliza masomo yao kwa mwaka wa Masomo wa 2021/ 2022 katika Cheti cha Uwakala wa Forodha Afrika Mashariki (CFFPC), Cheti cha Awali cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM), Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (DCTM), Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM), Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT).

Kwa Upande wa  Mhitimu  wa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi, Edwin Norasco amesema Siri ya ushindi alioupata ni kujituma na kuweka jitihada katika masomo kwa kutambua kilichompeleka chuoni hapo .

Ameeleza chuo ni kidogo hivyo ni fursa kwao kwani mazingira ya kusoma ni mazuri kwakuwa yanawapa fursa ya kuwa karibu na wakufunzi wao.

Ameongeza kuwa Taifa bado linahitaji wataalam wa kodi wao kama wahitimu wakiingia katika mamlaka wataweza kuwasaidia wafanyabiashara kuhakikisha wanafahamu sheria ya kodi.

Kwa upande wake Mhitimu wa Shahada ya Udhamiri ya Usimamizi wa Forodha na Kodi Glory  Sama amesema moja ya  changamoto katika kodi ni kutokuwa na uelewa kwa baadhi ya watu katika masuala ya kodi hivyo hakuna budi kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa wananchi.
Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Isaya Jairo akizungumza wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaama leo Novemba 25, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence  Mafuru akizungumza wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaama leo Novemba 25, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence  Mafuru akimtunuki cheti mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo kwa ngazi ya Stashahada ya uzamili katika kodi (PGDT)Groly Sama wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaama leo Novemba 25, 2022. 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence  Mafuru akitoa zawadi kwa Moja ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo chuoni hapo.


Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 15 ya chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2022 jijini Dar es Saalm.
Baadhi ya wakufunzi wakiwa katika Mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 15 ya chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2022 jijini Dar es Saalm.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad