HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 25, 2022

MKUTANO WA 42 WA CHAMA CHA WAONGOZAJI NDEGE TANZANIA(TATCA) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkutano huo umefanyika leo Novemba 25, 2022 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julias Nyerere na kuhudhuriwa na wajumbe wa TATCA, Wajumbe wa Chama cha Waongozaji Ndege Kenya (KATCA), Wajumbe wa Chama cha Waongozaji Ndege Uganda (UGATCA), Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, wawakilishi wa vyama vingine vya usafiri wa anga Tanzania (TAISOA na TATSEA) pamoja na Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUGHE Bi. Jackline Ngoda.

Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa TCAA Bw. Daniel Malanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 42 wa mwaka wa Chama cha Waongozaji Ndege Tanzania (TATCA). Bw. Malanga alifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA.
Kaimu Rais wa Chama cha Waongozaji Ndege Tanzania (TATCA) Bw. Limis Makoloela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 42 wa mwaka wa chama hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la TCAA (TUGHE) Bi. Jackline Ngoda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 42 wa mwaka wa Chama cha Waongozaji Ndege Tanzania (TATCA).

Picha ya pamoja 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad