HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 10, 2022

Benki ya Absa kutoa huduma bora zaidi zinazokidhi mahitaji ya wateja

 



Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Melvin Saprapasen ( wa tano kushoto), Meneja wa Absa Tawi la Ohio, Ally Janja (kushoto kwake), wafanyakazi wa Absa pamoja na Wateja wakigonganisha glasi kutakiana afya njema na mafanikio katika moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Katika maadhimisho hayo viongozi wa ngazi za juu wa benki hiyo walitembelea matawi ya Absa nchini kote ili kuzungumza na wafanyakazi na pia Wateja wao ili kuweza kuona namna bora ya kuwahudumia na kushughulikia mahitaji yao.

 
Wafanyakazi wa Benki ya Absa Tawi la Alpha House pamoja na Wateja wao wakitakiana afya njema na mafanikio katika hafla iliyoandaliwa na tawi hilo kwa wateja wao, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

 Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, John Beja (katikati, mwenye tai nyekundu) Mkurugenzi wa Fedha wa Absa Tanzania, Obedi Laiser (nyuma ya Beja), wakiselebuka pamoja na wafanyakazi na wateja wa Tawi la Absa Mikocheni, kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita



Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Zanzibar, Rabia Abood (katikati), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wake, Jabir Alfarsy katika hafla kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi hilo visiwani humo hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa wateja Maalum katika tawi hi
lo, Salim Salum.



Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Pugu, Heri Sijaona (kushoto), akizungumza na wateja wa benki hiyo tawini hapo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, katika hafla ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.



Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Slipway, Veronica Okio (kulia), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wake katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam hivi karibuni.

Meneja wa Kitengo cha Bima wa Benki ya Absa Tanzania, Sandeep Chavda (kushoto), akimpa zawadi mmoja wa Wateja wa Absa Tawi la Dar City, huku Meneja wa tawi Hilo, Winford Mwang'onda akiangalia, katika hafla ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo, Dar es Salaam hivi karibuni


Mmoja wa watumishi waliofanyakazi kwa muda mrefu katika Benki ya Absa Tawi la Tanga, Mwanajumaa Darweshi (wa pili kulia), akionesha cheti cha shukurani muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Absa Tanzania, Ndabu Lilian Swere (kushoto), katika hafla iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi hilo, mjini Tanga juma lililopita. Wa pili kushoto ni Meneja wa tawi hilo, Gloria Mallya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad