Mganga Mkuu wa Serikali Awaasa Watafiti wa Afya Kuzingatia Kanuni, Maadili ya Tafiti - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 10, 2022

Mganga Mkuu wa Serikali Awaasa Watafiti wa Afya Kuzingatia Kanuni, Maadili ya Tafiti

  MGANGA Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe ametoa wito kwa Watafiti wa afya kuzingatia kanuni na maadili ya utafiti wa afya ili kuleta matokeo chanya na yenye ushahidi wa kitafiti yatakayowezesha watunga sera na viongozi kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya ulinzi na ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa.


Ameyasema hayo leo wakati akifungua Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022. Amesema mafunzo hayo mafunzo hayo ni kwaajili ya Kuwajengea ujuzi na maarifa watumishi na wajumbe wa kamati za maadili ya udhibiti wa ubora wa tafiti za afya kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki ili waweze kuzingatia uadilifu katika utafiti na kutatua changamoto zinazojitokeza.

Mafunzo hayo yanatolewa na Mradi wa Muungano wa Udhibiti wa Utafiti wa Kitabibu na Uwezo wa Maadili katika Ukanda wa Afrika Mashariki (CCRREEA) ambao unashirikisha nchi tano ambazo ni Tanzania, Malawi, Kenya, Rwanda, na Uganda.

Amesema mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kuimarisha uwezo wao katika kuzingatia kanuni za maadili ya utafiti za kitaaluma na ya kisheria pamoja na usimamizi bora wa tafiti za afya.

Pia ameziasa Taasisi za kitaaluma nchini zitoe mafunzo yatakayosaidia kuongeza wataalamu wenye ujuzi wa kufanya tafiti zenye kuzingatia kanuni za maadili.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Dkt. Willium Siza amesema kuwa Mafunzo hayo ni mhimu sana katika nchi zinazofanya tafiti za magonjwa ya binadamu kwani yanaakisi majukumu ya taasisi za tafiti na yanajenga uwezo kwenye mfumo mzima wa wa utafiti hapa nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Taifiti za magonjwa ya Binadamu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Khadija Yahaya Malima amesema kuwa wanataka kuweka vipaumbele, misingi, taratibu na kanuni za pamoja katika nchi hizo tano ili kuleta ufanisi wa ufanyaji tafiti.

Amesema matatizo ya afya yameongezeka na inashindikana kutoa huduma za afya kwa kila mtu kwani wananchi hawana bima za afya ambazo zitamwezesha kupata huduma hivyo tafiti ni njia moja wapo ya kuboresha huduma na matibabu ya binadamu." Amesema Dkt. Malima

Amesema katika nchi hizo tano magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameongezeka na zinatafutwa njia bora za kudhibiti magonjwa hayo. Amesema pamoja na tafiti lakini tafiti hizo zinatakiwa kumlinda mwananchi anayefanyiwa utafiti ili asidhirike kwa namna yeyote ile kwani tafiti ni majaribio.

Licha ya hayo amesema kuwa tafiti zinapofanyika utaalamu wa ufanyaji tafiti zisivuke mipaka na ufanyike kwa kulinda afya ya mgonjwa kwani kunadawa nyingine zinamadhara kwahiyo anayefanya tafiti za Magonjwa lazima azingatie afya ya Mfanyiwa tafiti.

Amesema kunamagonjwa ya kuambukiza katika nchi hizo tano lazima washirikiane kulinda mipaka ya nchi hizo ili magojwa yasisambae kwa haraka na yadhibitiwe kabla hayajaenea kwa eneo kubwa

Kwa kuzingatia afya, haki za binadamu na kuzingatia kanuni za afya , malengo ya wizara na nchi kwa ujumla.

Mradi huo unafadhiliwa na European and Developing Countries Clinical Trials Partnership (EDCTP).

Na mradi huo wa CCRREEA ni wa miaka mitatu, ulianza rasmi Januari 2021 na unalenga kuboresha kanuni na maadili ya tafiti za kitabibu (clinical research) na uwezo wa udhibiti tafiti hizo.
MGANGA Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022.
Mtafiti Mwandamizi na Mkuu wa kitengo cha Maabara ya Sayansi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)-  Mabibo pia Mkuu wa Mradi wa Muungano wa Udhibiti wa Tafiti za kitabibu na Uwezo wa Maadili katika Mradi wa CCRREEA, Mwanaidi Kafuye akizungumza wakati wa Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022.
Mwakilishi kutoka Uganda akizungumza wakati wa Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022.
Mwakilishi kutoka Malawi kizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Dkt. Willium Siza kizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Taifiti za magonjwa ya Binadamu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Khadija Yahaya Malima akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022.
Renatha Sirro kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Utendaji bora na udhibiti wa tafiti za Afya (GRRP) yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022.


Baadhi ya washiriki wakisikiliza ufunguzi wa mafunzo jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad