MAMLAKA ZA MAJI NCHINI ZATAKIWA KUZINGATIA MIONGOZO INAYOTOLEWA NA EWURA KUBORESHA HUDUMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 10, 2022

MAMLAKA ZA MAJI NCHINI ZATAKIWA KUZINGATIA MIONGOZO INAYOTOLEWA NA EWURA KUBORESHA HUDUMA

 

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Mamlaka za Maji Safi na Usafi Mazingira.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mha. Modestus Lumato amewataka watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na EWURA ili kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo yao.

Mha. Lumato ametoa maelekezo hayo leo 10.10.2022, jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa watendaji hao,  yaliyolenga kuwajengea uwezo katika maandalizi ya mikakati ya utendaji ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

“Kama mlivyoelekezwa awali, kuja na  mikakati yenu inayozingatia miongozo iliyotolewa na EWURA, mafunzo haya yatawawezesha kuboresha mikakati hiyo itakayoongeza ufanisi wa utendaji wenu”. Alisisitiza Lumato.

Naye Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira EWURA, Mha. Exaudi Fatael, ameeleza kuwa, EWURA imeandaa miongozo husika kwa lengo la kuimarisha huduma hususani katika kudhibiti majanga, kudhibiti upotevu wa maji pamoja na namna bora ya kuchagua, kufunga, kupima na kutunza dira za maji sanjari na muongozo wa kushindanisha utendaji wa mamlaka za maji.

Watendaji wa jumla ya mamlaka  za maji 31 kutoka mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Tabora,Singida,Iringa, Kilimanjaro, Tanga, Manyara na Morogoro wanashiriki mafunzo hayo yatakayofanyika  kwa siku 4 (10-13 Oktoba 2022), ofisi za Makao Makuu ya EWURA jijini Dodoma.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA Mhandisi Modestus Lumato akifungua mafunzo kwa watedaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira Leo 10/10/22 jijini DodomaMkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA Mha.Exaudi Fatael akitoa neno la ukaribisho kwa watendaji waliohudhuria mafunzo hayo( hawamo kwenye picha hii)

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Mamlaka za Maji Safi na Usafi Mazingira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad