HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 28, 2022

SERIKALI MSIMU WA KILIMO 2022/2023 YAUTENGEA MKOA WA SINGIDA MGAWO WA MBEGU BORA ZA ALIZETI

 




Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro akijitambulisha katika uzinduzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiendesha trekta wakati akifungua kongamano la uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 Wilaya ya Iramba uliofanyika katika Uwanja wa Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Septemba 27, 2022. Anayeshuhudia uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro na kulia mwenye kaunda suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda.
Meneja wa TFRA Kanda ya Kati, Joshua Ng'ondya (kushoto) akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba namna ya kununua mbolea kwa mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda.

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Malietha Kasoga akitoa taarifa ya maendeleo ya kilimo na umwagiliaji.



Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda. akizungumza wakati wa uzinduzi huo.



Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akihutubia wakati akifungua kongamano hilo la siku mbili.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akijitambulisha katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akimkabidhi mbolea mmoja wa wakulima aliyeinunua kwa njia ya mfumo wa kimtandao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akipata maelezo wakati alipokuwa akikagua banda la mbegu la Seedco.

Ukaguzi wa mabanda ukiendelea.
Wadau wa kilimo wakiwa kwenye uzinduzi huo.




Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba na wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba na wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengiakizungumza kwenye uzinduzi huo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Mwalimu Ephrahim Kolimba akizungumza kwenye uzinduzi huo.


Wadau wa kilimo wakisubiri kuelezea shughuli zao katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU) Yahaya Khamis akizungumza.
Wakulima wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Kwaya ya Kizazi kipya ikitoa burudani. Kutoka kushoto ni Imani Mazala, Grace Tito, Ester Shila, Ester Samuel Emanuel Peter na Benjamin Kasanga.




Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora.
Uzinduzi ukiendelea.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakulima.


........................................

Na Dotto Mwaibale, Iramba




SERIKALI katika msimu wa kilimo wa 2022/2023 imeutengea Mkoa wa Singida mgawo wa mbegu bora za alizeti aina ya Certified 1 zenye ruzuku ya Serikali kilogram 500,000 zenye thamani ya Sh.2,500,000,000 ambapo bei kwa kilo moja sasa itakuwa ni Sh.5,000 badala ya Sh.8,000.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati akifungua kongamano la uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 katika Uwanja wa Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Septemba 27,2022.

Alisema pia Serikali itatoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima wote watakaojiandikisha kwenye mfumo maalum wa kupata ruzuku ambapo kwa sasa zoezi la usajili linaendelea katika halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida na kuwa bei ya mbolea yenye ruzuku iliyotangazwa na Serikali kwa mfuko wa kilo 50 kwa mbolea ya UREA ni Sh.70,000 kutoka Sh.124,734, DAP Sh.70,000 kutoka Sh.131, 676, NPKs Sh.70,000 kutoka Sh.122, 695, CAN sH.60,000 kutoka Sh.108, 156 na mbolea ya SA mfuko wa kilo 50 ni Sh.50,000 kutoka Sh.82,852.

Alisema Mkoa wa Singida kwa bajeti ya mwaka 2022/2023 umetengewa fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu katika miradi ya umwagiliaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.

Akizungumzia lengo la kongamano hilo alisema ni kuunga mkono na kutekeleza kwa vitendo jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuinua na kuthamini mchango wa kilimo hapa nchini.

"Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa moyo wa dhati ameongeza bajeti ya kilimo kutoka Sh.294.1 Bilioni hadi Sh.751.1 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 155.34" alisema Serukamba.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya kilimo, umwagiliaji na ushirika Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Malietha Kasoga alisema kwa msimu wa 2022/2023 wilaya hiyo imepanga kutekeleza Agenda 10/30 ya kuwainua wakulima na wafugaji kwa asilimia 10 hata kabla ya kufikia mwaka 2030 hiyo ni pamoja na kutekeleza agizo la Rais la kuweka msukumo kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara yakiwemo mazao ya kimkakati ya alizeti, pamba na mtama ili kukidhi mahitaji ya ndani na ziada kwa ajili ya soko la nje.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda alisema changamoto kubwa ni soko la mazao ya kilimo hasa zao la dengu ambapo hivi sasa bei yake kwa kilo ni Sh.830 bei ambayo haina tija kwa mkulima.

Aidha Mwenda alisema wilaya hiyo imetenga Sh.8 Bilioni kwa ajili ya kutengeneza skimu za umwagiliaji ekari 6,000 katika eneo la Masimba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad