Bondia nyota wa Tanzania
Ibrahim Class ametamba kumchapa mpinzani wake Gustavo Pina Melgar kutoka
Mexico katika pambano la kimataifa lililopangwa kufanyika Ijumaa
(Septemba 30) kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Pambano hilo
limeandaliwa na kampuni ya MO Boxing, ikiwa ni mara ya kwanza kwa
kampuni hiyo chini ya mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji.
Class
alisema kuwa baada ya kukaa nje ya ulingo kwa muda mrefu, ameamua
kurejea kwa kasi kwa lengo la kutwaa mikanda mbalimbali ya ngumi za
kulipwa nchini.’
Alisema kuwaamejiandaa vyema kwa ajili ya
pambano hilo na hatamdharau mpinzani wake kwani anaamini naye amekuja
kwa ajili ya ushindi. “Najua Melgar ni bondia mzuri lakini si kwa
kufikia kwangu, nimejiandaa vyema na nimuonyesha jinsi gani Tanzania ina
mabondia wazuri na wenye vipaji vikubwa,” alisema Class. Kwa upande
wake, Melgar alisema kuwa amekuja kusaka ushindi ili kuboresha rekodi
yake katika ngumi za kulipwa.
Mratibu wa pambano hilo kutoka MO
boxing Ahmed Seddiqi alisema kuwa maandalizi yamekamilika na ambapo
kutakuwa na mapambano sita ya utangulizi.
Pambano la kwanza la
utangulizi litakuwa kati ya bondia nyota wa Ghana, Alfred Lamptey ambaye
atapambana na bondia Abraham Ndauendapo kutoka Namibia huku Juma Choki
akizichapa na bondia wa kutoka Mexico Jose Hernandez ambapo bondia
kutoka Kenya Nicholas Mwangi atapimana ubavu na Emmanuel Mwakyembe wa
Tanzania.
Pambano lingine litakuwa baina ya bondia Sameer Anwar
dhidi ya Adam Mrisho huku Mwinyi Mzengelaakizichapana Sabari J na
pambano lingine litakuwa baina ya Lulu Kayage dhidi ya Sadra Mohamed.
Pambano
hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Azam TV, Boxer, MO XTRA, Mlimani City,
KCB Bank, White Sands Resorts, Bajaj na OTAPP. Kwa upande wake, Mkuu wa
Masoko na Uhusiano wa benki ya KCB, Christine Mnyenye alisema kuwa
wanajisikia fahari kubwa kudhamini mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
“Tunajisikia
fahari kubwa kudhamini mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini ikiwa si
mara etu ya kwanza, tutatumia mchezo huu kutambulisha huduma yetu ya
mpya ya bima na kuwaomba wadau wa ngumi za kulipwa na watu wengine
kujiunga nayo ili kujiwekea kinga na majanga mbalimbali,”alisema
Mnyenye.
Mratibu
wa pambano la kwanza la kampuni ya MO Boxing Ahmed Seddiqi (Katikati)
akiwatambulisha mabondia Ibrahim Class wa Tanzania (kushoto) na Gustavo
Pina Melgar wa Mexico ambao watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Mlimani
City Mratibu
wa kampuni ya MO Boxing Ahmed Seddiqi (katikati) akiwatambulisha
mabondia Ibrahim Class (watatu kushoto) na Gustavo Pina Melgar wa
Mexico (wa tatu kulia) kuelekea pambano la Ijumaa (Septemba 30) kwenye
ukumbi wa Mlimani City. Wa kwanza kushoto ni Fauqiya Shareer wa benki
ya KCB akifuatiwa na Ashish Josh wa Bajaj ambapo wa kwanza kulia ni
Salim Salim wa JustFit na Mkii wa Masoko na Uhusiano wa benki ya KCB
Christine Manyenye.
.
Mratibu wa pambano la kwanza la kampuni ya MO Boxing Ahmed Seddiqi
(Katikati) akizungumza katika mkutano wa kuwatambulisha mabondia ambao
watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Mlimani City Ibrahim Class (kushoto) na Gustavo Pina Melgar wakiwa katika uso kwa uso
Wednesday, September 28, 2022

Class atamba 'kumkalisha' Mmexico Mlimani City.
Tags
# HABARI MICHEZO
HABARI MICHEZO
Labels:
HABARI MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment