Mchezaji
wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania ' Taifa Stars" Feisal
Salum maarufu Feitoto akizungumza kwa njia ya video Call na Mlinda
mlango wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Aishi Salum Manula aliyeko nchini Libya.Manula ni Balozi wa Kampuni ya
Tigo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwashauri Watanzania kushiriki
kikamilifu Promosheni hiyo ili kupata nafasi ya kwenda kushuhudia
michuano ya Kombe la Dunia
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KAMPUNI
inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi Maisha ya kidijitali,
Tigo Tanzania , leo imetangaza ushirikiana baina ya Tigo Pesa na
HISENSE (Mshirika Rasmi wa kombe la Dunia la FIFA) Kuingia katika hatua
ya pili ya kampeni yake ya wakishua inayojulikana kama wakishua Twenzetu
Qatar na Hisense.
Kampeni hii ambayo itadumu kwa muda wa siku
120 imepamba moto zaidi hivi karibuni kufuatia uzinduzi wa kimkakati wa
ushirikiano kati ya Tigo na Boomplay katika uzinduzi wa hatua ya kwanza
ya kampeni ya wakishua.
Kupitia kampeni ya wakishua twenzetu
Qatar na Hisense, wateja wa tigo watakuwa na nafasi ya kushinda furushi
la vifaa vya nyumbani kutoka Hisense , zawadi za papo kwa papo za dakika
na SMS kwa wateja wote ambao watanunua kifurushi chochote kupitia Tigo
pesa.
“Tanzania ina mapenzi makubwa kwenye mpira wa miguu, ili
kuimarisha zaidi juhudi zetu za kuongeza ushirikishwaji wa kifedha
nchini, uamuzi wa ushirikiano huu na kampuni ya HISENSE umechangiwa kwa
kiasi kikubwa na ufahamu wa uwepo wa wapenzi wa mpira na kuwapa wateja
wetu ambao wanafanya miamala kupitia Tigo pesa fursa ya kwenda kutazama
mechi kubwa zaidi duniani, pia wateja watapata dakika 50 na SMS 200
watakapo nunua kifurushi cha thamani ya Tshs 500 na kuendelea kupitia
Tigo pesa” Amesema Angelica Pesha Afisa mkuu wa Tigo pesa.
Pesha
alibainisha ya kwamba Tigo pesa ni mtoaji huduma kamili wa huduma za
kifedha na tunaona fahari kuwazawadia wateja nafasi ya kutazama mechi
kubwa ya kimataifa ya mchezo wa mpira wa miguu kwasababu ni mchezo
mashuhuri zaidi nchini Tanzania. Kupitia aina mbalimbali
zilizorahisishwa za mifumo ya huduma za kifedha.
Amesema wateja
wana nafasi ya kushinda zawadi babu kubwa zinazoweza kubadilisha maisha,
ikiwemo tiketi 50 kwenda kuangalia mechi moja kwa moja nchini Qatar au
furushi la vifaa vya nyumbani ikiwemo smart Tv, Sound bar, Jokofu na
Microwave kutoka Hisense. “Tunaona fahari kuingia katika ushirikiano na
kampuni ya Tigo.
“ Tunatambua kwamba watanzania wanapenda mpira
na tunataka kuwapa watu fursa ya kupata furaha ya kipekee maishani
mwao.Kombe la dunia ni tukio la kukumbukwa na tunataka Tanzania nzima
kushiriki na sisi kufurahia tukio hili la kipekee” Anaeleza Jason Xu
Meneja Mauzo wa Hisense.
Miamala ya Tigo pesa ikiwemo kulipia
bidhaa na huduma kupitia lipa kwa simu, lipa bill, malipo ya serikali,
kutuma pesa, kuweka fedha, kuhamisha fedha kutoka benki, kupokea fedha
kutoka mahali popote duniani na nyingine nyingi zitampa nafasi mteja
kuingia katika droo ya wiki inayotarajia kupata washindi 80 ambapo 50
kati yao watashinda safari iliyolipiwa ya kwenda Qatar na wengine 30
watapata furushi la vifaa vya nyumbani kutoka Hisense.
Hivyo ili
kushinda nafasi hii ya pekee maishani ya kusafiri na zawadi nyingine,
tunawahamasisha wateja kufanya miamala mingi kadri wawezavyo kupitia App
ya Tigo pesa au piga *150*01#
Kwa upande wakeBalozi wa kampuni
hiyo, Kiungo wa Klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa
Stars', Feisal Salum 'Feitoto' amesema kampeni hiyo itawaleta mashabiki
pamoja kuchangamkia fursa ya kuwenda kushuhudia fainali hizo za mwezi
Novemba.
"Kampeni hii imekuja wakati muafaka, watanzania wengi
wanafuatilia mpira, wanafuatilia mashindano mbalimbali, sasa mbele yetu
kuna fainali za kombe la Dunia, Tigo na Hisense wamekuja kuwasaidia
mashabiki wenye bahati wanaotumia huduma ya Tigopesa, ninwakati wa
kutumia huduma.zao kuweza kujishindia nafasi hizi," amesema Feitoto.
Amesema
katika kampeni hiyo anashirikiana na Balozi mwingine, golikipa wa Simba
na Taifa Stars, Aishi Manual ambaye kwa sasa yupo na timu hiyo nchini
Libya.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo sambamba na Hisense kutoa zawadi kwa Feisal Salum 'Feitoto' pamoja na mmoja ya waandishi aliyeshinda drooo iliyochezeshwa wakati wa uzinduzi huo iliyoshirikisha waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
No comments:
Post a Comment