WIZARA YAAHIDI KUALIKA WASHIRIKI WENGI ZAIDI WA NJE KATIKA MAONESHO YA SABASABA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 9, 2022

WIZARA YAAHIDI KUALIKA WASHIRIKI WENGI ZAIDI WA NJE KATIKA MAONESHO YA SABASABA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk amesema kuwa Wizara pamoja na balozi zake, itaendelea kuhamasisha nchi marafiki na mashirika ya kimataifa kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) ambayo amesema yanazidi kuimarika ukilinganisha na miaka ya nyuma.


Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 08 Julai 2022 alipotembelea maonesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Julius Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar Es Salaam.

Balozi Mbarouk amesema kuwa kushiriki kwa wageni wengi kutoka nje ya nchi, kuna faida kubwa kwa wafanyabiashara wa hapa nyumbani, kwa kuwa kuna wapa fursa ya kujifunza teknolojia mpya, kupata masoko ya bidhaa wanazozizalisha na wabia wa kushirikiana nao katika biashara na uwekezaji.

Akiwa kwenye viwanja hivyo, Mhe. Naibu Waziri alitembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho hayo, hususan wale wa kutoka nje ya nchi ili kujionea bidhaa, huduma na teknolojia walizokuja nazo. Katika maongezi na washiriki hao alisisitiza umuhimu wa kubadilishana teknolojia na uzoefu na wafanyabiashara wa hapa nchini ili kujenga uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zitakazokuwa na uwezo wa kukabili ushindani wa soko la dunia.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Joseph Sokoine aliahidi kuwa Wizara yake itashirikiana na wadau wengine kama Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wengi zaidi kutoka nje ya nchi wanashiriki maonesho hayo. “Wizara yetu ni mdau mkubwa katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na maonesho ni jukwaa muhimu katika diplomasia ya uchumi, hivyo tutaongeza nguvu zaidi kushajihisha kampuni nyingi zaidi kutoka nje, zishiriki maonesho haya mwakani na miaka mingine”, Alisema Balozi Sokoine.

Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya mwaka 2022 yalianza tarehe 28 Juni na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai 2022 ambapo nchi 20 zinashiriki kwa kuoenesha bidhaa, huduma na teknolojia mbalimbali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika Bnada la Wizara ya Mambo ya Nje lilipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba). Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akipewa maelezo kuhusu ushiriki wa Wizara katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa katika moja ya banda yaliyopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba)
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisikiliza maelezo ya mshiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kutoka nje ya nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba)

KATIBU MKUU KATIKA MAONESHO YA SABASABA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwa kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kwa ajili ya kutembelea mabanda mbalimbali kujionea bidhaa, huduma na teknolojia..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika Bnada la Wizara ya Mambo ya Nje lilipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akipewa maelezo kuhusu ushiriki wa Wizara katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisalimiana na Balozi wa Marekani hapa nchini ambaye alifika kutembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje lilipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (SabasabaNo comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad