MTANDAO WA TeIW KUWEZESHA WAWEKEZAJI KUPATA TAARIFA ZA TAASISI ZOTE ZA SERIKALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 8, 2022

MTANDAO WA TeIW KUWEZESHA WAWEKEZAJI KUPATA TAARIFA ZA TAASISI ZOTE ZA SERIKALI

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe akimueleza fursa za Uwekezaji zilizopo nchi nchini, Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi, Shaka Hamdu Shaka alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam Julai, 2022.


Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe akimueleza fursa za Uwekezaji zilizopo nchini, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam Julai, 2022.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46, Katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Saba saba jijini Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama ametembelea banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuelezwa na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa (TIC), Pendo Gondwe kuhusiana na Majukumu mbalimbali ambayo Wizara inafanya na pia fursa za Uwekezaji zilizopo nchini. 

Aidha Dkt. Tamatama ameshukuru TIC kwa jitihada wanazofanya katika sekta ya Uvuvi hususani suala la kuhakikisha wawekezaji wanapata stahiki zao za msingi wanapojisajili na TIC katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar-es-Salaam 6 Julai, 2022.


Baadhi ya wananchi wakipata elimu walipotembelea Banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46, Katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Saba saba jijini Dar Es Salaam.
Wafanyakazi TIC wakiwa katika Picha ya pamoja na Wananchi.

MTANDAO wa dirisha lina lojumuisha taasisi Mbalimbali za Serikali wa Tanzania Eletronic Investiment Window (TeIW), unatoa huduma mahali pamoja katika Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuzinduliwa Septemba, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TIC kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46, Katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Saba saba jijini Dar Es Salaam. Meneja Uhusiano na Mawasiliano TIC, Pendo Gondwe amesema kuwa Kunamfumo wa huo utatoa huduma kwanjia rahisi na haraka zaidi.

Amesema Kuwa dirisha hilo litahusisha taasisi 12 ambazo zinaingilia katika uwekezaji.

Taasisi hizo ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania( TIC), taasisi inayohusika na Vibali vya kufanya kazi (Work Permity), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Wizara ya Ardhi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA).

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Taasisi nyingine ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Uhamiaji.

Pendo amesema kuwa kutambulishwa Mfumo Mpya wa TeIW utakapo kamilika utasaidi na kurahisisha utoaji huduma mahali pamoja.

"Tupo Katika Banda la Wizara ya uwekezaji, Banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Kliniki ya biashara ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya biashara na Uwekezaji nchin." Amesema Pendo

Amesema kuwa Mwekezaji ataingia kwenye Kompyuta yake na kupata huduma tofauti tofauti kwa pamoja katika mfumo wa dirisha moja.

Kwahiyo tunatarajia kwamba huu Mfumo ya kutoa huduma mahali pamoja lazima kuwa pamoja ili Mwekezaji apate taarifa pamoja.

Licha ya Hayo amewashukuru wateja na Viongozi mbalimbali waliotembelea banda la Uwekezaji, viwanda na Biashara na kujipatia elimu.

Pendo amesema kuwa wamejipanga katika mabanda matatu tofauti kwaajili ya kutoa elimu, Fursa mbalimbali kwenye Sekta Kuu za Vipaumbele zinazopatikana hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad