SIKU YA BATIKI TANZANIA YAZINDULIWA DAR, BATIKI KUFUNGUA UCHUMI WA MWANAMKE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 8, 2022

SIKU YA BATIKI TANZANIA YAZINDULIWA DAR, BATIKI KUFUNGUA UCHUMI WA MWANAMKE

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza leo Julai 8, 2022, wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Batiki Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi Roijok Progress Centre, Rose Urio akizungumza leo Julai 8, 2022, wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Batiki Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Wanawake wakiwa katika uzinduzi wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Batiki Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam leo Julai 8, 2022.Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza leo Julai 8, 2022, wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Batiki Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akipokea Batiki leo Julai 8, 2022, wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Batiki Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.


TAASISI isiyo ya kiserikali ya Roijok Progress Centre ikishirikiana na Serikali wamezindua Siku ya Batiki Tanzania ambayo itafufungua Milango ya Uuzaji wa Batiki Bora nje ya Nchi na ndani ya Nchi.

Akizungumza leo Julai 8, 2022, Mkurugenzi wa Taasisi Roijok Progress Centre, Rose Urio wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Batiki Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Uzinduzi huo ulikuwa na lengo la Kuitanga Batiki ndani na Nje ya Nchi.

Amesema uzinduzi huo utafungua Masoko ya Batiki pamoja na akuwaunganisha wazalishaji wa Batiki Tanzania kuwa na masoko ya ndani na nje ya Nchi.

Tumefanya hii kwa msaada Mkubwa wa Serikali, tumekuwa na Viongozi wa Serikali ambao wamekuwa sababu kubwa ya sisi kufikia hapa.

Amesema kuwa Maisha yamebadilika thamani ya mwanamke ni kuweza kujitegemea kiuchumi ingawa Manamke anamajukumu makubwa ya kulea familia, lakini Mapinduzi Makubwa yaliyotokea dunia hivyo mwanamke anakila sababu ya kuingia kwenye uchumi.

Amesema Batiki ni bidhaa inayoweza kuzalishwa hata eneo dogo lenye uwazi. "Kwahiyo sisi Kama Roijok kupitia mradi wetu wa Batiki utasaidia kuanzia wazalishaji wadogo mpaka wenye Viwanda."

Amesema Lengo ni wanawake kuweza kuzalisha lakini pia kusimamia Familia.

Amesema katika Mradi wa Batiki wanampango wa kuzindua Ua la Mama ambalo litakuwa kwaajili ya Kumuenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani.

Rose amesema katika Ua la Mama Katikati wataweka nembo ya madini ya Tanzanite ikiwa ndio madini pekee yanayopatikana Tanzania.

Lakini Katika Mradi huu Rose amasema wanaenda Kuboresha na kupata Batiki zenye Viwango na Kupata Batiki zenye vipimo vyenye uwiano sawa.

"Katika Mradi huu tunaenda kuboresha Standard za Batiki.....Hatuna Standard ya Batiki Mwingine ana mita mbili ns Nusu, mwingine ana tatu Mwingine nne kwahiyo tunaenda kupata standard ya Batiki.... Amesema Rose.

Amesema na Baada ya kupata viwango vinavyohitajika itasaidia kujiuza na kupata masoko mengine mengi makubwa.

Rose amesema kuwa maono yao ni kuona Batiki nikuona zikiwasaidia akinamama kiuchumi, ikiongeza pato la Taifa lakini pia tunapoongelea Uchumi na Batiki iwepo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali ipo kazini kwa ajili ya kuwakomboa wanawake katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kukata mzizi wa fitina kwa kutaka kumuona mwanamke akiwa na furaha siku zote na ipo tayari kuwasaidia wanawake na vijana katika shughuli zao mbalimbali.

"Rais Samia ana lengo la kuwakomboa wanawake na kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kuwakopesha fedha kutoka katika halmashauri." Amesema Dkt. Doroth

Pia amesema licha ya Rais kuwashika mkono wanawake na vijana pia wizara itaendelea na utaratibu wa kuwawezesha wanawake katika kuzalisha bidhaa zao.

Dkt .Dorothy amesema asilimia 75 wanaozalisha batiki ni wanawake na vijana hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwekeza katika makundi hayo.

"Tutaweka siku maalumu ya uvaaji Batiki ambayo itakuwa ni kila Julai 8 ambapo kila mtanzania anatakiwa kuvaa vazi la batiki." Amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad