Na.Catherine Sungura, WAF-Dodoma
Jumla
ya watoto 12,131,049 sawa na asilimia 117.8 wamepatiwa chanjo ya matone
dhidi ya ugonjwa wa Polio kwa watoto chini ya miaka mitano kati ya
watoto 10,295,316 waliolengwa kwenye kampeni ya Chanjo iliyofanyika
nchini tarehe 18 hadi 21 Mei mwaka huu.
Hayo
yamebainishwa leo na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati akitoa
tathimini ya kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya Ugonjwa wa Polio kwa
watoto chini ya miaka mitano nchini kwenye viwanja vya Bunge jijini
Dodoma.
Waziri
Ummy amesema idadi hiyo iliyofikiwa ni mafanikio makubwa kama nchi na
kutoa pongezi kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya,Timu za uendeshaji wa huduma
za afya ngazi ya Mikoa na Halmashauri ,watumishi wa afya pamoja na wadau
mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo kwa kusimamia kikamilifu
maandalizi ,uzinduzi na utekelezaji wa kampeni katika maeneo yao kwa
umahiri mkubwa.
"Nawapongeza
pia wazazi na walezi wote kwa kuitikia wito wa Serikali kwani afua ya
chanjo ni muhimu kwa watoto katika kuwalinda dhidi ya magonjwa yanayo
zuilika kwa chanjo".
Waziri
Ummy aliutaja Mkoa wa Ruvuma umeongoza kwa kuvuka lengo kwa 131%,
ikifuatia na Shinyanga 128%, Rukwa 123%, Pwani 122%, Arusha 122%, Mbeya,
Geita, Dar es Salaam na Simiyu yote ina 121%, Singida, Dodoma na Tabora
118% , Kigoma, Njombe, Katavi 117%, Morogoro 116%, Mara, Mtwara, Lindi
na Tanga 115%, Kilimanjaro na Mwanza 114%, Manyara na Iringa 113%,
Songwe na Kagera 111%.
Hata
hivyo Waziri Ummy ametoa wito kwa Viongozi,wadau na wazazi kutoa
ushirikiano kwa kampeni zinazofuata ambazo zinatarajiwa kufanyika mwezi
Julai na Agosti mwaka huu.
Ameongeza
kuwa tunayo kila sababu ya kuilinda nchi yetu na watoto wetu dhidi ya
ugonjwa wa Polio.'Mzazi/Mlezi hakikisha watoto wanapata chanjo ya
Polio,bado tunaweza kutunza rekodi ya Tanzania kuwa nchi isiyokuwa na
ugonjwa wa Polio duniani.
Kampeni
ya Polio inatakiwa kufanyika kila baada ya wiki nne ili kuhakikisha
watoto wote wanafikiwa kulingana na mwongozo wa WHO wa kukabiliana na
ugonjwa wa Polio unaelekeza kuwa endapo mlipuko wa ugonjwa umetoke nchi
ambayo mlipuko umetokea pamoja na zile zinazozunguka zinapaswa kufanya
kampeni za kutoa chanjo ya polio mara nne mfululizo pamoja na kutoa
chanjo kwa watoto wote walio chini ya miaka mitano ili kuzuia kusambaa
kwa maambukizi ya ugonjwa huu.
No comments:
Post a Comment