HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2022

UVIKO 19 BADO UPO MIONGONI MWETU WATAALAMU WA AFYA WASISITIZA


Na Mwandishi Wetu
KUPITIA kampeni kuhamasisha uchanjaji wa chanjo ya UVIKO19 inatekelezwa na Amref Health Africa Tanzania wataalamu mbalimbali wa afya wamekuwa wakizungumza juu ya UVIKO19 pamoja na chanjo.

Katika moja ya mahojiano na Dkt. Elisha Osati Akizungumza kuhusu kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa Korona nchini pamoja na kwamba hali inaonekana kutulia kwa sasa.

Dkt. Osati ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani alisema kutokana na takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa na Wizara ya Afya inaonyesha ugonjwa bado upo miongoni mwetu na Hospitali zetu bado zinapokea wagonjwa wa UVIKO19.

Dkt.Osati aliendea kusema kuwa kwa Sasa takriban asilimia 98 ya wagonjwa wote wanapokelewa Hospitalini ni wale ambao hawajachanja.

Hii inaonyesha kuwa wale waliochanja wameendelea kuwa salama zaidi dhidi ya UVIKO19.

Tungeendelea kuona nchi nyingine duniani zikipambana na ugonjwa huu kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kuchanja chanjo imebaki kuwa moja kati ya mbinu ambazo zimeonyesha matokeo mazuri hasa kwenye kupunguza wagonjwa pamoja na kasi ya kusambaza kwa ugonjwa huu hatari na Korona.

Dkt.Osati ametoa wito kwa Watanzania wote kutopuuzia suala la chanjo ikiwa kwa sasa suala la chanjo ikiwa kwa sasa bado hatujamaliza ugonjwa huu ndani ya nchi yetu.

Amesisitiza kuwa chanjo hizi zinazotolewa hapa nchini katika Hospitali zote pamoja na vituo maalumu ni salama na kinga yake inaweza kutusaidia hata pale ambapo kirusi kinaweza kukibadilisha na kuja katika mfumo mpya (New Variant).

Amref Health Africa Tanzania wameendelea kuwa mstari wa mbele kufikisha elimu kwa watanzania juu ya ugonjwa huu hatari na namna ambavyo watu wanaweza kujikinga Ili kubaki salama wao na wapendwa wao.

Taarifa hizi zimekua zikisambazwa nchi nzima kupitia mitandao ya kijamii na vyanzo vingine vya habari mtandaoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad