HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2022

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAWAFUNDA WABUNGE MIKAKATI YA KUKABILIANA NA WANYAMA WAKALI NA WAHARIBIFU

 

Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya semina kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu uhifadhi wa wanyamapori nchini na namna ya kukabiliana na changamoto za migongano kati ya binadamu na wanyamapori.
Akizungumza katika semina hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Wizara yake haifurahishwi na matukio yanayotokana na wanyama wakali na waharibifu.

“Hata sisi wizara hatufurahishwi kuona wananchi wanateseka kutokana na changamoto ya wanyama wakali na waharibifu kwa sababu wengine wanapoteza maisha au kupata ulemavu.” Mhe. Masanja amesisitiza.

Aidha, amesema Serikali ina mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto hizo ikiwamo kuweka maboya katika maeneo ambayo wavuvi wanavua samaki ili kuonyesha mipaka ya hifadhi na kuangalia namna ya kuboresha kifuta jasho/machozi.

Mhe. Masanja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za UVIKO 19 ambazo zitatumika kwa ajili ya kuchimba mabwawa ndani ya hifadhi ili wanyama waweze kupata huduma ya maji na kuacha kuingia katika makazi ya watu.

Naibu Waziri Masanja ameahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad