Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeomba kibali cha kuajiri askari wa uhifadhi wapya 600 ambao watasambazwa kwenye maeneo hatarishi ili kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja
(Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali
la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Jacqeline Ngonyani Msongozi, aliyetaka
kujua mpango wa Serikali wa kuwadhibiti tembo wanaovamia, kuharibu mazao
na kujeruhi wananchi katika kata za Mindu, Kalulu na Tinginya, Wilaya
ya Tunduru.
Mhe.
Masanja ameongeza kuwa Wizara ina mkakati wa kuanzisha vituo vya
kikanda vya Askari katika maeneo yenye changamoto ya wanyamapori wakali
na waharibifu.
Pia,
amesema Serikali itatoa mafunzo kwa askari wa wanyamapori wa vijiji; na
kuelimisha wananchi kuhusu namna bora ya kupunguza athari zinazotokana
na wanyamapori wakali na waharibifu.
Katika
hatua nyingine, akijibu swali kuhusu mikakati ya Serikali ya kutangaza
maporomoko ya Kalambo Mhe. Masanja amefafanua kuwa Wizara itatumia
vyombo vya habari, itaandaa machapisho na majarida na kushiriki katika
maonesho, matamasha, matukio na makongamano ya utalii na biashara
yanayofanyika ndani na nje ya nchi ili kutangaza kivutio hicho.
Pia
amesema njia ya kuweka mabango katika viwanja vya ndege ikiwemo uwanja
vya ndege wa Songwe na maeneo mengine katika Mkoa wa Rukwa itatumika
kutangaza utalii huo.
No comments:
Post a Comment