HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 10, 2022

KUSAINIWA KWA ITIFAKI YA MABORESHO YA USAFIRI WA ANGA KUFUNGUA FURSA BAINA YA TANZANIA NA MAREKANI

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright wameongoza zoezi la kihistoria la kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kufunguliwa kwa safari za moja kwa moja za Usafiri wa anga baina ya nchi hizo mbili.
 
Hafla hiyo ya kusaini mkataba huo ilivyohudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Gabriel Migire, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S.Johari na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) Musa Mbura.
 
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Waziri Mbarawa alisema maboresho hayo ya itifaki ya mkataba ambao awali ulisaini Agosti mwaka 2000 ni sehemu sasa ya fursa mpya za usafiri baina nchi mbili , ongezeko la abiria pamoja na kukuza biashara na uchumi. Na kuongeza kuwa sasa anaamini kwa fursa hiyo shirika la ndege nchini(ATCL) na mashirika mengine ya ndege yaliyosajiliwa nchini yataichangamkia. 
 
"Kufikiwa kwa azma hiyo ya kuwa na usafiri wa anga wa moja kwa moja kati ya Marekani ni matokeo chanya ya ziara ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan nchini Marekani na uzinduzi Filamu ya Royal Tour" Alisema Mbalawa

Kwa upande wake Balozi Wright alisema hafla hiyo inahitimisha safari ya miaka takribani 22 ya Kihistoria tangu Marais wa Tanzania na marekani ambao ni  Benjamin Mkapa na Bill Clinton kutia saini mkataba wa ushirikiano wa usafiri wa Anga Agosti mwaka 2000 nchini Tanzania sambamba na mazungumzo baina ya Rais Samia na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris Aprili 15,2022 nchini Marekani na Sasa ndoto ya kuwa na anga la pamoja inafikiwa. 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TCAA Hamza Johari alisema wao kama wataalam Sasa jukumu lao ni kukamilisha masharti baina ya pande hizo mbili na hatimaye kufungua rasmi fursa na kuongeza kuwa mkataba huo ni wa aina yake kwani unaruhusu aina mbalimbali za ndege, miruko mingi na hata uwezo mbalimbali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia) pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright(kushoto) wakionesha itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia) pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright(kushoto) wakisaini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia) pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright(kushoto) wakibadilishana itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi  Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadu mbalimbali wa Usafiri wa Anga wakati hafla ya kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright akizungumza na  wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga pamoja na waandishi wa habari  wakati hafla ya kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi  Profesa Makame Mbarawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA),Hamza S.Johari akitoa neno la shukrani kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania pamoja na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Usafiri wa Anga wakifuatilia zoezi la utiaji saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia) akiagana na Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright(kushoto) mara baada ya kumaliza zoezi la kusaini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad