HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 10, 2022

SABAYA NA WEZAKE SITA WAACHIWA HURU


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha Leo Juni 10, 2022 imewaachia Huru Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na Wenzake sita baada ya kutowakuta na hatia kwenye kesi ya Uhujumu uchumi Namba 27/2021.

Hukumu hiyo imetolewa leo June 10,2022 na Hakimu wa mahaka ya Hakimu Mkazi Arusha, Patricia Kisinda.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kisinda amesema Mahakama imepitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili na imeona ushahidi uliotolewa na upande wa Jamuhuri ulikuwa na Mashaka na uliigubikwa na Maswali yasiyokuwa na Majibu

Aidha ameongeza kuwa hati ya mashataka ilikuwa na Mapungufu makubwa kisheria.

kutokana na Sababu hizo akasema Mahakama amewaachia Huru Washtakiwa wote na Upande ambao hautaridhishwa na Maamuzi una Nafasi ya Kukata Rufaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad