KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA PILI YA HAYATI MKAPA KUFANYIKA ZANZIBAR JULAI 13-14, 2022 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2022

KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA PILI YA HAYATI MKAPA KUFANYIKA ZANZIBAR JULAI 13-14, 2022

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya - Senkoro kizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Juni 29, 2022, wakati wa kutambulisha kumbukizi ya pili ya hayati Mkapa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya - Senkoro kizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Juni 29, 2022, wakati wa kutambulisha kumbukizi ya pili ya hayati Mkapa kufanyika Zanzibar Julai 13-14,2022. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uongozi wa Mkapa katika Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Rita Kahurananga na kulia ni Meneja Tathmni na Ufatiliaji wa Miradi Rahma Musoke wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

 Meneja Tathmni na Ufatiliaji wa Miradi Rahma Musoke wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation akifafnua miradi iliyofanywa na taasisi yao tangu kufariki dunia kwa Hayati  Rais Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya - Senkoro na wakwanza kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Uongozi wa Mkapa katika Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Rita Kahurananga.
JUKWAA la kumbukizi ya pili ya aliyoyafanya na kuacha alama muasisi wa Taasisi ya wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa linatarajia kufanyika Zanzibar Julai 13 na 14 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Juni 29, 2022, wakati wa kutambulisha kumbukizi ya pili ya hayati Mkapa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya - Senkoro amesema kuwa Jukwaa hilo limepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar.

Kauli mbiu ya Jukwaa hilo ni “Uongozi Madhubuti Hamasa ya Mabadiliko kwa Wote.” (Resilient Leadership- Inspiring Change for All).

Jukwaa au Mdahalo huo wa siku mbili utaanza saa Mbili asubuhi na unatarajia kumalizika saa nane mchana huku wageni waalikwa takriban 500 watahudhiria Siku ya kwanza mdahalo utafunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Othman Masoud.

Na siku ya pili ya Julai 14,2022 itakuwa siku ya kilele cha mdahalo huo kwa mwaka 2022, na Mgeni rasmi katika siku hii muhimu atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Ellen amesema kuwa Katika siku hizo mbili kutakuwa na mdahalo kuhusu mada kuu mbili ambazo ni

1.Kuongoeza kasi katika mikakati ya mabadiliko katika mifumo ya afya Tanzania kupitia biashara ushirika, (Accelerating Strategic Health Transformation in Tanzania through Business Coalition)

2.Ubunifu katika miradi na mikakati yaa ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi za umma na za binafsi katika kuleta huduma ya afya kwa wote. (Innovative Public-Private Partnerships (PPP) approaches towards attaining Universal Health Coverage)

“Kupitia mada hizi washiriki watapata fursa ya kusikia mijadala ya juhudi za mashirikianao ya Serikali za Tanzania Bara na Visiwani, Sekta binafsi na Wadau wa maendeleo na pia iliyoendelea kuchagizwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa, katika kuimarisha mifumo ya afya kwa lengo la kuhakikisha kila mtu popote alipo anapata fursa ya kupata huduma bora za afya. Mjadala huu pamoja na mambo mengine utashirikisha jopo la wadau watakao chambua kwa undani umuhimu wa biashara ama uwekezaji wa pamoja katika kuinua afya na ustawi wa kila mmoja wetu.” Amesema Dkt. Ellen

Viongozi wengine wa kitaifa watakaohudhuria mdahalo huu ni pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Daktari Hussein Ali Mwinyi, ambae pia ni “msarifu” wa Taasisi ya Mkapa Foundation, aliyerithi nafasi ya Hayati Benjamin Mkapa katika Taasisi yetu kuanzia Desemba 2021.

Wageni wengine watakaoshiriki hafla hii ni pamoja na Viongozi wakuu wa Serikali, Marais na Viongozi wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa Nchini, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Sekta binafsi na za Umma,Wanafamilia na Marafiki wa Hayati Benjamin Mkapa kutoka ndani na Nje ya Nchi, pamoja na Asasi za kiraia na Viongozi wa dini.

"Tunapenda kutoa shukrani kwa wadau wote ambao wapo Pamoja na sisi katika maandalizi ya kufanikisha mdahalo huu wa kumbukumbu na kuenzi Maisha ya Hayati Mheshimiwa Benjamin William Mkapa,Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania na Msarifu wa Taasisi Benjamin William Mkapa." Amesema Dkt. Ellen

Kwa upande wake, Meneja wa Usimamizi na Tathimini na Ufuatiliaji wa Miradi ya Taasisi hiyo, Rahma Musoke amesema hadi sasa kupitia ‘Program’ zake Taasisi ya Benjamin Mkapa imefika watu Milioni 26 kupitia Miradi yake mbalimbali kwenye Mikoa yote ya Tanzania.

Musoke amesema Miradi hiyo inalenga makundi tofauti katika kuboresha utoaji huduma za Afya, hata hivyo katika Sekta ya Afya wamepeleka Watumishi katika vituo mbalimbali kupitia wadau wa maendeleo na michango ambayo inapatikana sanjari na kuajiri Watumishi na kuwapeleka katika maeneo mbalimbali.

“Watumishi zaidi ya 10,042 tumewaajiri hadi sasa na kuwapeleka katika vituo mbalimbali kutoa huduma za Afya, ambao wapo kwenye maeneo ya Vijijini ni 5882 na wengine wanatoa huduma katika ngazi ya vituo”, amesema Musoke.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad