HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2022

KIKAO CHA WABUNGE WA DAR ES SALAAM NA MAWAZIRI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akieleza jambo wakati wa kikao na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuhusu mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo kuelekea kwenye Bajeti Kuu ya Serikali, kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (Mb) akielezea masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara wakati wa kikao na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuhusu mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo kuelekea kwenye Bajeti Kuu ya Serikali, kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma, kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kulia ni Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) akieleza jambo wakati wa kikao na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuhusu mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo kuelekea kwenye Bajeti Kuu ya Serikali, kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.
Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Abbas Tarimba, akizungumzia maendeleo ya jimbo lake, wakati wa kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa TAMISEMI na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.
Mbunge wa Kigamboni na Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Faustine Ndungulile, akifafanua jambo wakati wa kikao na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuhusu mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo kuelekea kwenye Bajeti Kuu ya Serikali, kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.
Kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad