Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango
tarehe 31 Mei 2022 amewasili Stockholm nchini Sweden ambapo anatarajia
kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 utakaofanyika
tarehe 2 hadi 3 Juni 2022 nchini humo.
Dhumuni la mkutano huo ni
kuchochea utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (Ajenda
2030) hususani katika upande wa mazingira na kujadili namna ya kurejesha
uchumi endelevu katika kukabiliana na janga la Uviko 19. Aidha mkutano
huo ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kufanyika mkutano wa kwanza wa
mazingira wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Stockholm mwaka 1972.
Mkutano
wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na
Serikali kutoka mataifa mbalimbali pamoja na wadau wa Mazingira Duniani.
Wednesday, June 1, 2022

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWASILI NCHINI SWEDEN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment