HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 9, 2022

DKT. STERGOMENA AMTEMBELEA JENERALI MBOMA

 WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amemtembelea Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali (Mstaafu) Robert Philemon Mboma nyumbani kwake Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumjulia hali.

Waziri Stergomena amemtembelea Jenerali Mbona akiwa ni mwendelezo wa utaratibu wake aliojiwekea wa kuwatembelea na kufanya Mazungumzo na wastaafu hao tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 12 Septemba, 2021 na kuapishwa rasmi 13 Septemba, 2021.

Mhesmiwa Stergomena alianza utaratibu huo, kwa kumtembelea Mkuu wa Majeshi wa Kwanza, Jenerali (Mstaafu) Mirisho Sami Hagai Sarakikya, akifuatiwa na Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Msuguri na Jenerali (Mstaafu) Davis Adolf Mwamnyange.

Wakuu wa Majeshi waliowahi kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) tangu kuanzishwa kwake Septemba 01, 1964 ni pamoja na Jenerali (Mstaafu) Mirisho Sami Hagai Sarakikya (1964 - 1974), Marehemu Jenerali Abdallah Twalipo (1974 – 1980), Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Msuguri (1980 - 1988), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (1988 -1991), Jenerali (Mstaafu) Robert Philemon Mboma (1991 - 2001), Jenerali (Mstaafu) George Mwita Waitara (2001 - 2007), Jenerali (Mstaafu) Davis Adolf Mwamunyange (2007 - 2017) na Jenerali Venance Salvatory Mabeyo (2017 - sasa).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad