HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 9, 2022

RAIS SAMIA AWATAKA WANANCHI WA MKOA WA KAGERA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI ZILIZOPO

 




RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Mkoa wa Kagera una fursa kubwa ya kiuchumi na kibiashara, hivyo unapaswa kupewa kipaumbele katika mipango na mikakati ya maendeleo.

Rais Samia amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Aidha, Rais Samia amesema, Mkoa wa Kagera ni wa kimkakati katika kuinua uchumi wa nchi kwa kuwa unapakana na nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa onyo kwa Vyama vya Ushirika kuacha kunyonya wakulima wa kahawa mkoani humo na kuwaacha wauze mazao yao kulingana na bei wanayoitaka.

Rais Samia pia, amesema bei ya mauzo ya kahawa haipaswi kuwa na makato kwa kuwa Serikali inatoa ruzuku katika pembejeo.

Halikadhalika, Rais Samia amewataka Waziri wa Ardhi pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi kushughulikia changamoto ya uhaba wa malisho na uwepo wa migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo mkoani humo.

Kuhusu uvuvi, Rais Samia amesema Serikali inafanya jitihada ya kuinua sekta ya hiyo ikiwemo kununua boti na kuongeza fedha kwenye mfuko wa uvuvi kwa wavuvi wadogo ili kuwakomboa kuwainua kiuchumi.

ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad