HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 26, 2022

ASILIMIA 76.14 YA TABIA ZA KIBIDAHAMU CHANZO CHA AJALI ZA BARABARANI

 

 

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Leopord Fungu akizungumza wakati warsha ya utoaji wa taarifa pamoja na kupata maoni kutoka kwa wadau wa usalama barabarani iliyoandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Amend.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Leopord Fungu  akizungumza wakati warsha ya utoaji wa taarifa pamoja na kupata maoni kutoka kwa wadau wa usalama barabarani iliyoandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Amend. kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo akizungumza wakati wa warsha hiyo kulia ni Meneja Mkuu wa Amend Tanzania Simon Kalolo
Meneja Mkuu wa Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza wakati wa warsha hiyo
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga akizungumza wakati wa warsha hiyo


NA OSCAR ASSENGA, TANGA.



ASILIMIA 76.14 ya tabia za kibinadamu zimetajwa kama mojawapo ya vyanzo vikuu vinnne ambavyo vinasababisha ajali za barabarani na hivyo kupelekea kupoteza maisha au kupata majeraha ikiwemo kupoteza mali.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Leopord Fungu wakati warsha ya utoaji wa taarifa pamoja na kupata maoni kutoka kwa wadau wa usalama barabarani iliyoandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Amend.

Ambapo alisema ni vyema watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wengine watumie matumizi sahihi ya bara bara ili kuepusha athari mbalimbali ambazo wanaweza kuzipata ikiwemo ajali zinazotokana na kutokuwa makini.

Fungu alisema tabia hizo za kibinadamu zimesababisha kupelekea kwa asilimia kubwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa na kama vitazingatiwa ajali zitapungua na hivyo kuondokana na ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikiondoa nguvu kazi ya Taifa.

“Madereva kuendesha vyombo vya moto bila mafunzo ya usalama barabarani hii sio sawa na wengi wanapenda nyia za mkato kujifunza na tabia hizo tukiziacha zitatusaidia kupunguza ajali “Alisema RTO huyo.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa serikali,watendaji wakiwemo madiwani katika maeneo yao kama kuna watu wanaoendesha boda boda wahakikishe kwamba wanakuwa wamepata elimu ili kuwapeusha na ajali.

Awali akizungumza Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo alitoa wito kwa wafanya biashara katika halmashauri ya jiji la Tanga ambao wanatumia barabara kuweka bidhaa zao kuacha mara moja kufanya hivyo.

Meya huyo alisema vitendo hivyo sio sawa hata kidogo lazima waheshimu taratibu zilizowekwa ikiwemo kuacha kupanga bidhaa zao kwenye maeneo ya maegesho ya barabara na kuvuka milango mlikodishwa na kuweka barabarani ambazo ni matumizi ya vyombo vya moto.

“Wapita njia tafadhali msitumie njia za watumia kwa miguu kuweka bidhaa zenu lakini tiini sheria bila kushurti kwa kuziiondoa bidhaa hizo kila mtu ajue mipaka ya milango wake na bidhaa zilizoingia barabara kuacha mara moja kwa lengo la kuepukana na ajali zinazoweza kujitokeza“Alisema

Awali akizungumza wakati wa warsha hiyoMkurugenzi Mtendaji wa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Sipora Liana alisema watatoa wataendelea kushirikiana huku wakiwashukuru kwa kuendelea kuweka miundombinu kwenye maeneo yote katika Jiji la Tanga.

Alisema yeye kama mdau iwapo shirika hilo linataka kuweka miundombinu na bodaboda watengewe maeneo mazuri yatayowezesha kufanya kazi zao vizuri na waweke mtandao utakaofanya wajulikane pindi linapotokea tatizo.

Hata hivyo Meneja Mkuu wa Amend Tanzania Simon Kalolo alisema lengo la warsha hiyo ni kutoa mrejesho wa nini ambacho kimefanyika kwa miaka mitatu iliyopita wakizungumzia elimu kwa shule za Msingi,Miundombinu.

Alisema kwamba wameamua kuweka alama kwenye maeneo mengi ya shule katika Jiji la Tanga ili kuweza kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika .

“Tumekuwa tukiweka alama za aina mbalimbali barabarani,tumeanza jitihada mbalimbali kwenye shule zenye mahitaji maalum zinahitaji nguvu zaidi kwa kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa alama na wamekuwa hawajui"Alisema Kalolo

Alisema pia kuboresha barabara kuwa rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu hasa watoto mafunzo ya madereva kwa waendesha boda boda ambao wamekuwa wakisababisha ajali nyingi nchini na Tanga kwa hiyo warsha hiyo ilikuwa ni kupata maoni na mapendekezo.

Hata hivyo alisema baadae ili kuweza kuona suala la usalama barabara linavuka na kuona waboreshe mipaka iliyozoelekeza kuhakikisha wanatokoeza ajali za barabarani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad