Asila Twaha , TAMISEMI
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David
Silinde amesema, Serikali inaendelea kutafuta rasilimali ili barabara ya
mvumi Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ijengwe kwa kiwango kwa Lami kwa
urefu wa km tatu.
Mhe.
Silinde ameyasema hayo leo Mei 25, 2022 wakati wa ziara yake ya kukagua
barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kilometa 1 kuanzia eneo la
makaburini hadi bilia kata ya mvumi mission Halmashauri ya Wilaya ya
Chamwino Jijini Dodoma.
Wakati
wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Mvumi Mhe. Livingstone Lusinde
aliwasilisha ombi la wananchi wake kutaka kuongezewa barabara ya lami
ili kuongeza hadhi ya Kata hiyo na kurahisisha shughuli za usafirishaji.
Mhe.
Silinde amesema suala hilo litafanyiwa kazi na atahakikisha anasimamia
utekelezaji kwa vitendo ili barabara hiyo ipate lami ya kutosha kuipa
hadhi Mvumi kuwa mji mdogo.
“Tuendelee
kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan na kumuunga mkono ili aweze kufanya mambo makubwa zaidi kama
mnavyoona kwenye utekelezaji wa miradi na sisi wasimamizi wake
tutaendelea kuisimamia kwa vitendo niwahakikishie mvumi mtaongezewa lami
zaidi ya kilomita 2.
Aidha
Mhe. Silinde amesema ameridhishwa na ukaguzi aliofanya katika barabara
hiyo kwa kuwa asilimia kubwa umekamilika na amemuelekeza Meneja Wakala
wa Barabara za Mjini na Vjijini TARURA kuandaa bajeti ya uwekaji wa taa
za kwenye barabara hiyo .
“Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
ametuagiza sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMI tunapojenga barabara tuweka na
taa za barabarani niwaelekeze TARURA hili tutalisimamia” amesema Mhe.
Silinde
Naye
Mbunge wa Jimbo la Mvumi Mhe. Livingstone Lusinde, amemshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Rais –TAMISEMI kwa
kuhakikisha wanaisimamia TARURA kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa
barabara na ameishukuru Serikali kuridhia ombi la wananchi kuongezewa
kilomita za lami.
“Sisi
wananchi wa mvumi pamoja na maendeleo tunayo yaona Serikali inayofanya
lakini pia tumejiandaa kwa ajili ya zoezi la sensa kuhesabiwa
linalotegemewa kuanza nchi nzima mwezi Agosti,2022 na niombe Serikali
iendelee kutuunga mkono kuleta maendeleo hapa Mvumi ” amesema Mhe.
Lusinde
No comments:
Post a Comment