HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 30, 2022

TRA YAWAHIMIZA WANANCHI KUHAKIKI UBORA WA VINYWAJI KABLA YA KUTUMIA ILI KULINDA AFYA ZAO.

 

 Ni katika kampeni ya “Hakiki Stempu, Linda Afya Yako” ambayo imezinduliwa katika siku za hivi karibuni na Mamlaka ya Mapato Tanzania. TRA imewekeza na kufanya maboresho makubwa katika mifumo ya TEHAMA yenye lengo la kuongeza ufanisi, uwajibikaji, uwazi na kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Eneo mojawapo ambalo maboresho hayo yamefanyika ni katika stempu za Kodi za kieletroniki (ETS). Stempu hizi ni alama maalum inayobandikwa au kuchapishwa katika bidhaa ili kuonesha kuwa bidhaa hiyo ni halali na imezalishwa au kuingizwa nchini na mfanyabiashara anayetambulika na imelipa kodi ya ushuru wa bidhaa stahiki. Mfumo huu wa stempu za kielektroniki umeunganishwa na mifumo ya TRA ili kupata takwimu sahihi za uzalishaji/uagizwaji kwa maana ya idadi, ujazo pamoja na kodi halisi inayostahili kutozwa. 

TRA inapenda kuwahamasisha wananchi wanaotumia bidhaa hizo kushiriki kulinda afya zao kwa kutambua bidhaa halisi na halali kwa matumizi kwa kutumia simu zao za kiganjani kabla ya kuzitumia bidhaa hizo. Watumiaji wanaweza kuzitambua bidhaa halali kabla ya kuzitumia kwa kupakua App ya Hakiki Stempu wenyewe kwenye simu zao bure na kufuata maelekezo kama ambavyo tumeyatoa kuanzia leo kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ikiwa ni pamoja na televisheni, radio, magazeti mitandao ya kijamii na machapisho mbalimbali.

Kwa sasa, bidhaa zinazobandikwa Stempu za Kielektroniki za Ushuru ni bidhaa za Sigara, Mvinyo wa Zabibu, Pombe Kali, Bia, Mvinyo wa matunda mengine kama vile Ndizi, Rozela, Nyanya pamoja na aina zote za vileo. Bidhaa nyingine ni Vinywaji Laini kama Soda, Visisimuzi (energy drinks), sharubati (juice), Maji yanayowekwa kwenye chupa na Bidhaa za Muziki na Filamu zilizofungashwa kwenye CDs/DVDs/Kanda. Hadi sasa, viwanda ambavyo tayari vimeshaunganishwa na mfumo ya stempu za kieletroniki kote nchini ni 286 na waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi ni 106.

Faida mojawapo ya ETS ni kulinda afya ya mtumiaji kwa kujiridhisha kuwa bidhaa hiyo imezalishwa na nani, lini, na itakuwa imepita katika mikono ya vyombo vya udhibiti wa ubora vya serikali na kuhakikisha kwamba kodi halali ya serikali inalipwa kupitia kwa wazalishaji au waagizaji wanaotambulika tu na siyo wale wadanganyifu.

Faida nyingine ni kuwezesha kutambuaa na kuzuia bidhaa bandia sokoni kwa manufaa ya kuwalinda wafanyabiashara wema wanaotekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria.

Hivyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania inatoa wito kwa watumiaji na wananchi kwa ujumla kupakua App ya Hakiki Stempu kwenye simu zao za kiganjani bure ambayo itawawezesha kutambua bidhaa isiyofaa kwa matumizi kwa usalama wa afya zao pamoja na kuiwezesha serikali kukusanya kodi stahiki na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma zingine za jamii kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania. Vile vile inatoa wito kwa wazalishaji na waingizaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa kutumia mfumo wa ETS kwa uaminifu kwani mfumo huu una faida nyingi kwao ikiwemo kulinda bidhaa zao sokoni dhidi ya bidhaa bandia pamoja na kusaidia makadirio ya kodi kwa haki.

Katika kampeni ya “Hakiki stempu, Linda afya yako” iliyofanyika jijini Dar es salaam wiki iliyopita, mabalozi wa Kampeni hiyo walitoa elimu kwa watu wengi kuhusu umuhimu wa programu hii, kuwaonyesha jinsi ya kupakua programu, jinsi ya kuitumia, na umuhimu wa programu hii katika kuhakikisha watumiaji wa bidhaa wanaepuka matumizi ya bidhaa ambazo hazijathibitishwa ili kulinda afya zao. Lengo la kudhibiti ubora wa bidhaa za vinywaji ni kwa sababu kuna aina nyingi za vinywaji hivyo si rahisi kuelewa ubora wa vinywaji hivyo na pia kutambua kama ni salama kwa matumizi na pia kujua kama bidhaa hiyo imelipiwa kodi kihalali katika mamlaka ya mapato. Baadhi ya vinywaji hivyo ni kama vile mvinyo, pombe kali, juisi, maji na sigara n.k.

Kumekuwa na mwitikio mkubwa sana ambao ni chanya kwa watu wote tuliofikia na wameelewa kwa urahisi jinsi ya kutumia mfumo huu wa "hakiki stempu" kwani ndio njia rahisi zaidi.

1.      Wananchi wakifundishwa na kuhamasishwa kutumia  ETS Hakiki App  na kudownload kwenye simu zao  ili waweze kuhakiki vinywaji vyao ili walinde  afya yao na kuepukana na bidhaa fake

1.      Innocent Minja ETS project manager kutoka TRA akitoa mafunzo/ training kwa baadhi ya maafisa wa TRA kuhusiana na app ya Hakiki Stempu na jinsi ya kudownload na  kutumia app hiyo


1.      Maofisa wa TRA Tanga, wakiendelea na zoezi la Hakiki stempu katika jiji la Tanga

1.      Tabora


1.      Dar es salaam

1.      Maofisa wahamasishaji wa program ya Hakiki Stempu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kutoa elimu ya jinsi ya kupakua na kutumia App hiyo jijini Dar es salaam


 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad