WAKULIMA ZAIDI YA 5000 WILAYANI MPWAPWA WANAJIHUSISHA NA KILIMO HIMILIVU CHA MTAMA KUPITIA FARM AFRIKA NA WFP - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2022

WAKULIMA ZAIDI YA 5000 WILAYANI MPWAPWA WANAJIHUSISHA NA KILIMO HIMILIVU CHA MTAMA KUPITIA FARM AFRIKA NA WFP

 


Mmoja ya wakulima wa zao la Mtama ambao ni sehemu ya wanuifaika wa mradi wa Kilimo himilivu cha Mtama akiendelea kutoa majani yaliyoota kwenye shamba darasa ambalo amekuwa akilitumia kutoa elimu ya kilimo hicho kwa wakulima wengine.


Ofisa Mradi wa Kilimo himilivu cha Mtama Wilaya ya Mpwapwa kutoka Shirika la Farm Afrika  Adelina Ayubu ( kushoto) akifafanua jambo wakati akielezea kilimo hicho   kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) .Kulia ni Ofisa kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Laswai akiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Ofisa mradi wa Kilimo himilivu cha Mtama katika Wilaya ya Mpwapwa Adelina Ayubu ( wa kwanza kushoto)pamoja na Ofisa wa WFP ( wa pili kulia) wakiwa makini wakati yakitolewa maelezo kuhusu mradi huo walipotembelea shamba darasa.
Adelina Ayubu kutoka Shirika la Farm Afrika akielezea jambo kwa waandishi wahabari
Mmoja ya wakulima wa Kilimo himilivu cha Mtama akiwa na mkewe wakati wakielezea jinsi wanavyojihusisha na kilimo hicho wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Mwanahalisi Ally akizungumza na waandishi wa habari pamoja na maofisa  wa WFP na Farm Afrika ( hawapo pichani) baada ya kumtembelea ofisini kwake leo Machi 3,2022


Ofisa Mradi wa Kilimo himilivu cha Mtama Wilaya ya Mpwapwa wa Shirika la Farm Afrika Adelina Ayubu ( wa kwanza kushoto) akiwa makini kumsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Mwanahalisi Ally ( hayupo pichani) baada ya kufika ofisini kwake.Wengine kwenye picha hiyo ni waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Mwanahalisi Ally ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya maofisa kutoka WFP, Farm Africa na waandishi wa habari.
Ofisa Kilimo Wilaya ya Mpwapwa Edson Kileo( wa pili kulia) wakiwa wameshika mche wa mti na maofisa wa WFP na Farm Afrika


Na Said Mwishehe, Michuzi TV -Mpwapwa

OFISA Mradi wa Kilimo Himilivu cha Mtama katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kutoka Shirika la Farm Afrika Adelina Ayubu amesema kuwa zaidi ya wakulima 5000 katika wilaya hiyo wanajihusisha na kilimo hicho ambacho kimeonekana kuleta tija kubwa kwa wananchi kutoka kwenye vijiji 51, Kata 23.

Amesema hayo leo wilayani Mpwapwa wakati akielezea mradi huo wa mtama ambao wamekuwa wakiutekeleza kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP)pamoja na Ireland ambapo amefafanua mradi huo unatekelezwa sambamba na kutoa elimu katika vikundi vya wakulima ambapo inakuwa rahisi kuwafikia.

"Pia kupitia mradi huo, tumekuwa tukiwahasisha wakulima wa mtama kuzingatia masuala ya lishe kwa kulima bustani za mbogamboga nyumbani, lakini tunatoa elimu kuhusu namna ya kutunza mazingira kwa kutumia miti inayoitwa miti malisho.Kingine ambacho tunakifanya kupitia mradi huu ni tunawaunganisha wakulima na masoko,benki pamoja wadau wengine wa kilimo.


"Katika zana ya mikopo kwenye kutekeleza mradi kuna kipengele cha kuunganisha wakulima na hizi sekta mbalimbali ambazo si za Serikali, kwa hiyo tukaona ni vema tukashirikisha benki ili kuongeza kipato cha wakulima ambapo fedha watakazopata kutoka benki watazitumia kuandaa mashamba na mambo mengine yanayohusu kilimo.

"Kwa hiyo katika msimu wa kilimo uliopita benki ya NMB tuliwafuata kama mwanzo tu na walitusikiliza na wakatoa mikopo kwa vikundi vinne vinavyojihusisha na kilimo cha mtama, marejesho yalikuwa mazuri.Hivyo mwaka huu benki ya NMB imeamua kuongeza idadi ya vikundi ambavyo vitapatiwa fedha.Lakini tunaendelea kuzungumza na benki nyingine ikiwemo ya TADB,"amesema Adelina Ayubu.

Ameongeza mradi wa kilimo himilivu cha Mtama kinatekelezwa katika Wilaya Sita zilizopo mkoa wa Dodoma ambazo ni Kongwa, Bahi, Kondoa, Chemba,Mpwapwa na Chamwino."Kwa Wilaya ya Mpwapwa msimu uliopita tulizalisha tani za mtama mtama 13000 na bahati nzuri wakulima wengi wameelewa umuhimu wa kulima mtama, hivyo Farm Afrka na WFP tunaamini kadri mradi utakavyoendelea wengi watajiunga na kilimo hiki ambacho soko lake ni la uhakika."

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad