Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Amiri Msuya akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usindikaji wa Matunda na Mbogamboga
ambao unatekelezwa na Taasisi ya Dira Women Organazation (DIWO) kwa
kushirikiana na Stiftug Josef Vogt utawalenga vijana 150 wenye umri
kuanzia miaka 16 hadi 24 ambao watatoka kwenye shule ya Sekondari
Kicheba na vijana wanaoishi kwenye kata ya Kicheba. Mkurugenzi
wa Taasisi ya Dira Orgazation (DIWO) Shamsa Danga akizungumza wakati wa
uzinduzi wa mradi huo kulia ni Diwani wa Kata ya Kicheba Mkodingwa
kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu Kibaha
Diwani wa Viti Maalumu Kibaha akizungumza
Diwani wa Kata ya Kicheba Mkodingwa akizungumza jambo kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Orgazation (DIWO) Shamsa DangaDiwani wa Kata ya Mlingano akizungumza jambo
NA OSCAR ASSENGA, MUHEZA.
MRADI
wa Usindikaji wa Matunda na Mbogamboga umeelezwa kwamba utachangia kwa
asilimia kubwa kuinua uchumi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza kwa
kukusanya ushuru wake na kuweza kuongeza wigo wa mapato ikiwemo kodi ya
Serikali kuongezeka.
Mradi huo ambao unatekelezwa na Taasisi ya
Dira Women Organazation (DIWO) kwa kushirikiana na Stiftug Josef Vogt
utawalenga vijana 150 wenye umri kuanzia miaka 16 hadi 24 ambao watatoka
kwenye shule ya Sekondari Kicheba na vijana wanaoishi kwenye kata ya
Kicheba.
Utakwenda sambamba na utoaji mafunzo kwa vijana wa
shule za Sekondari Kata ya Kicheba wilayani humo na kwa wale waliopo nje
ya shule kuhusu masuala la ujasiriamali usindikaji wa mbogamboga ,usafi
wa majumbani pamoja na utunzaji wa bustani.
Hayo yalisemwa na
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Amiri Msuya wakati uzinduzi wa
mradi huo katika halfa iliyofanyika wilayani humo ambapo alisema ujio
huo utawasaidia sana vijana kuweza kujikwamua kiuchumi ikiwemo
kujiajiri.
Alisema baadaye wataona umuhimu na tija ya kuamua
kuanzisha viwanda vidogo vidogo na Halmashauri kutokana na kupata fedha
wanazokopeshwa kutoka kwenye mfumo wa vijana, wanawake na walemavu
asilimia 10 za mapato ya ndani
Aidha alisema baada ya vijana hao
kuweza kujua kuongeza thamani kwa mazao wanayosindika wanaamini
watapata ajira na kupunguza wimbi la ambao hawana ajira kwa kuwa
wataongeza thamani ya mazao na kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja
ikiwemo Halmashauri kuweza kukusanya ushuru na kuongeza mapato.
“Lakini
kutokana na kuongeza thamani ya mazao Halmashauri itaongeza mapato
kwani kuongezeka huko thamani itasaidia mazao yataweza kuonekana kwenye
supermaketi na kuweza kuuzwa nje ya nchi na kipato kitapaa kwa sababu
yale ambayo yalikuwa yakiharibika na kutupwa sasa yatakuwa yanauzika
“Alisema
“Niwashukuru sana Taasisi ya Diwo ujio wenu hapa Muheza
kwetu sisi ni kama Baraka na furaha kuona mnawasaidia vijana kwani
kupitia mradi huu utawawezesha hata wanapopata mikopo ya vijana asilimia
4 kutoka Halmashauri wataweza kuwa wabunifu na kubuni miradi yenye
tija”Alisema
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi
huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Orgazation (DIWO) Shamsa Danga
alisema mradi huo ni wa mwaka mmoja na upo kwa awamu tatu ambapo awamu
ya kwanza itakuwa ni usindikaji wa matunda na mbogamboga.
Shamsa
alisema awamu ya pili itakuwa ni utunzaji wa bustani na usafi wa
majumbani ambapo unatajwa utakuwa mkombozi kwa vijana waliopo wilayani
Muheza hususani Kata ya Kicheba ambapo utatekelezwa.
“Shughuli
za mradi ni utoaji wa mafunzo kwa vijana juu ya usindikaji wa chakula
kwa ajili ya uendelezi wa biashara kama njia na shughuli ya kujiingizia
kipata na yatahusisha ujuzi wa ufungashaji na kuongeza thamani ya bidhaa
zilizochaguliwa”Alisema
Alizitaja bidhaa hizo kama vile
Tomato Sauce,Chill Sauce,Pactin,Jam ya fenesi,Juice ya
fenesi,Viungo,Matunda yaliyokaushwa,Pickles,Fruits Jam,Crips na Pipi za
maganda ya Machungwa”Alisema Mkurugenzi huyo.
Akieleza sababu za
mradi huo kufanyika wilayani Muheza alisema kwa sababu ni eneo ambalo
lilibarikiwa kuwa na matunda ya aina mbalimbali na mbogamboga pamoja na
viungo.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kicheba B
Rajabu Juma alisema wameipokea kwa mikono miwil taasisi hiyo ambayo
imefika kwao wakati muafaka ambao watatoa mafunzo kwa vijana wao na
kwamba wataiunga mkono kwa kuhakikisha hata pale panapohitajika shamba
kwa ajili ya kilimo cha mbigambga halmashuri ya kijiji itakaa na kutoa
ushikiri wa kulifanikisha hilo.
Friday, March 4, 2022

MRADI USINDIKAJI MATUNDA NA MBOGAMBOGA KUINUA UCHUMI HALMASHAURI MUHEZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment