HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2022

KUKAMATWA KWA NYARA ZA SERIKALI PAMOJA NA GONGO LITA 570 NA WATUHUMIWA

 


Na.Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msadizi wa Polisi ACP
Justine Masejo ameviambia vyombo vya habari kuwa tarehe 02.03.2022
muda wa 07:30 mchana huko maeneo ya Ngarenaro katika halmashauriya
jijila Arusha askari Polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumi wa wawili
ambaoni AMANDA THOMAS (22) mkazi wa kwa Morombo na KELVIN
THOMAS (27) mkazi wa Ngarenaro wakiwa na nyama Pori ya mnyama
Pofu KG150.

Kamanda Masejo amesema kuwa uchunguzi wa awaliwa tukio hili
umebaini kuwa watuhumi wahao wamekuwa wakijihusisha na biashara
hiyo ya nyara za serikali ambapo uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana
na askari wanyama Pori ili kubaini mtandao wao.

Ameendelea kusema kuwa Katika tukio jingine tarehe 02.03.2022 muda wa
saa 09:30 alasiri huko kata ya RHOTIA tarafa ya mbulumbulu wilaya ya
karatu na Mkoa wa Arusha askari Polisi walifanikiwa kuwakamata
watuhumiwa wawili ambao ni PETRO GAUDENCE (57) mkazi wa
mbulumbulu na REVOCATUS PROTUS (28) mkazi wa mbulumbulu wa kiwa
na lita 570Ltr za Pombe haramu ya moshi (gongo).

ACP Masejo amewambia waandishi kuwa Operesheni kali inaendelea
katika wilaya zote ili kubaini wanaofanya biashara hizo, hivyo ni watake
baadhi ya watu wanaojihushisha na biashara hizo haramu ya gongo
Pamoja na nyara za serikali kuacha mara moja kwani hatuto muonea
muhari mtu yeyote anayejihusisha na biashara hizo haramu.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na upelelezi wa matukio nayo na
mara baada ya upelelezi kukamilika majalada hayo yatapelekwa ofisi ya
taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisherai.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa kila wananchi kuwa mlinzi na kulinda
rasilimali za nchi adhimu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi
juu ya uhalifu na wahalifu wanaohujumu rasilimali za Nchi ili hatua kali za
sheria zichukuliwe dhidi yao.


 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad