Mkuu
wa mkoa wa Arusha John Mongela akiwa na Afisa Maendeleo ya jamii mkoa
wa Arusha Blandina Nkini,wakitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu
ya maandalizi ya siku ya wanawake duniani machi 8
Na.Vero Ignatus,Arusha
Katika
kuelekea kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila
mwaka machi 8 siku hiyo hutolewa wito wa kuhakikisha uwezeshaji na
usawa wa Kijinsia
Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa mkoa
wa Arusha John Mongela amesema kuwa, Faida za usawa wa kijinsia sio tu
kwa wanawake na wasichana bali ni kwa kila mtu ambaye maisha yake
yatabadilika kutokana na dunia yenye usawa.
Mongela amesema
kuwa tarehe nne wanawake watatembelea wodi za kinamama katika hospitali
ya Levolosi na kufanya usafi kutoa misaada ya vifaa katika wodi za
kinamama,hivyo ni vyema watanzania wengine wakaungana nao katika
shughuli hiyo yenye tija katika jamii.
Amesisitiza kuwa amesema
kuwa usawa wa kijinsia unapaswa kupewa kipaumbele na ushiriki wa
wanawake katika maadhimisho hayo yatakayoenda sambamba na matukio kadhaa
hadi kilele.
Ameitaja Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya wiki ya
siku ya wanawake duniani "Haki usawa kwa maendeleo endelevu tujitikeze
kuhesabiwa"
Pia alibainisha kwamba tarehe 5 wanawake watapata
fursa ya kutembelea hifadhi ya Ngorongoro na Mgeni Rasmi atakuwa Mary
Masanja Naibu waziri Maliasili na Utalii sanajari na mbio za kilometa
tano na kumi kwa wanawake
Kwa Upande wake Afisa Maendeleo ya
jamii mkoa wa Arusha Blandina Nkini alifafanua kuwa mbio hizo mgeni
Rasmi atakuwa Pauline Gekul sanjari na Kongamano la wanawake
litakaloendeshwa na chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru.
Bi Nkini
amefafanua zaidi shughuli za siku hiyo kwamba siku ya tarehe 7
kutakuwa na maonesho ya watoa huduma za wanawake itakayoenda sambamba na
siku ya kilele uzinduzi wa kanzi data ya wanawake na uongozi Tanzania
Aitha
amebaisnisha kuwa Mgeni rasmi wa kilele cha maadhimisho ya siku ya
wanawake duniani atakuwa Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na
makundi Maalumu Doroth Gwajima.
Ikumbukwe kuwa Siku hiyo
ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa
kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya
haki za wanawake.
Siku hii pia huongeza chachu katika harakati
za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika
jamii. Aidha maadhimisho ya siku hiyo kwa mwaka huu yamebeba ujumbe wa
usawa kwa watu wote.
Siku ya wanawake duniani kwa mara wa kwanza
ilisherehekewa katika mwaka wa 1911 ambapo mataifa 11 yalikusanya
wanawake mia moja walipoanza kuadhimisha siku hii ambapo Mwaka 1908
jumla ya wanawake 15,000 waliandamana katika katika mji wa New York
wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi ,kupata ujira wa kuridhisha na
kupewa haki ya kupiga kura
Mwaka 1909 mwanamke kwa jina la Clara
Zetkni alipendekeza kuanzishwa kwa siku ya wanawake duniani katika
mkutano wa wafanyakazi wanawake uliofanyika katika jiji la copenhagen
nchini Dermark
Friday, March 4, 2022

RC MONGELA: USAWA WA KIJINSIA SIYO KWA WANAWAKE PEKEE BALI KWA KILA MTU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment