*******************
Na. Catherine Sungura,WAF-Dodoma
Tanzania
na Israel kushirikiana katika kuboresha huduma za Magonjwa ya moyo kwa
watoto kupitia Shirika la SACH linalojishughulisha na huduma za
magonjwa hayo kwa watoto nchini humo
Akiongea wakati wa kikao
hicho leo kilichofanyika jijini Dodoma kati ya Wizara ya afya na
Mtendaji Mkuu wa Shirika la huduma za magonjwa ya moyo kwa watoto (Save a
Child’s Heart – SACH Bw. Simon Fisher, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Prof. Abel Makubi amesema kuwa wamekubaliana kuendeleza ushirikiano
katika masuala yanayohusiana na huduma hizo hapa nchini.
“Kikao
hiki kilikua na lengo la kujadiliana maeneo ambayo Wizara ya Afya
inaweza kushirikiana na shirika la SACH katika kuongeza idadi ya
wataalam watakaopata mafunzo ya muda mfupi na ya muda mrefu nchini
Israel katika Ubingwa na Ubingwa bobezi wa magonjwa ya moyo kwa watoto”.
Aidha, Prof. Makubi amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa kutoa
huduma za moyo kwa watoto kupitia kambi za matibabu hapa nchini kuanzia
mwaka 2015.
Prof. Makubi alisema kuwa Shirika hilo imekwishatoa tiba kwa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya Moyo wapatao 130.
Aidha,
alimuomba mtendaji huyo kupeleka kambi za matibabu kwenye Hospitali
nyingine za Rufaa za Kanda na Mikoa ili kusogeza huduma karibu na
wananchi.
“Tunakushukuru kwa kuwezesha Shirika la SACH kwa
kuipa kipaumbele nchi ya Tanzania katika kutoa mafunzo ya muda mfupi na
muda mrefu kwa wataalam wetu wa hapa nchini kwenye eneo la tiba za
magonjwa ya Moyo ikiwemo huduma za upasuaji kwani kupitia huduma hizo
Serikali imeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kupunguza
idadi ya wagonjwa waliokuwa wakipewa rufaa ya kutibiwa nje ya
nchi”Aliongeza Prof. Makubi.
Licha ya mashirkiano hayo katika
upande wa magonjwa ya Moyo kwa watoto na mafunzo Katibu Mkuu huyo
hakusita kumuomba Mtendaji huyo kuongeza idadi ya wanufaika wa mafunzo
ya huduma zinazotolewa kupitia Taasisi ya SACH ili kuboresha huduma
katika eneo hilo pamoja na kuisaidia Tanzania kutoa mafunzo kwa wataalam
katika huduma za kibingwa za magonjwa ya dharura na huduma kwa wagonjwa
mahututi ambapo ujenzi wa miundombinu kwenye vituo vya kutolea huduma
za afya umekamilika.
Naye, Mtendaji Mkuu wa SACH BW. Simon
Fisher amesema kuwa Shirika lake litaendelea kushirikiana na Wizara ya
Afya katika kuimarisha huduma za magonjwa ya Moyo kwa watoto hapa nchini
na kuahidi kufanyia kazi maeneo ya ushirikiano yaliyojadiliwa na pande
zote mbili wakati wa kikao hicho.
Akiwa hapa nchini Mtendaji
Mkuu huyo ametembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma
kwa lengo la kujionea hali ya utoaji huduma katika Hospitali hiyo na
pia kupata uelewa juu ya mahitaji ya mafunzo ya Kibingwa na Ubingwa
bobezi kwa wataalam wa hospitali hiyo kwenye eneo la huduma za magonjwa
ya Moyo kwa watoto.
Wednesday, March 30, 2022

TANZANIA NA ISRAEL KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA ZA MAGONJWA YA MOYO KWA WATOTO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment