Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mbunge
wa Jimbo, la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanya ziara ya kushtukiza
kwenye Ujenzi wa Kituo Cha Afya Kongowe ,kitakachogharimu Tsh Mil .400 hadi kukamilika kwake.
Akiwa
katika eneo la tukio, Koka amezisisitiza kamati za usimamizi wa Ujenzi
huo kuwa wazalendo na kuheshimu pesa ya serikali huku akihimiza miradi
kukamilishwa kwa wakati lengwa.
Hata hivyo amewataka wajumbe wa kamati hizo na Viongozi kusimamia Ujenzi sambamba na kuzingatia thamani ya pesa.
Koka
alieleza, kituo hicho kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya
Halmashauri ya Mji Kibaha, ambapo kinatarajiwa kukamilika Julai Mwaka
huu na kuwanufaisha wakazi wa kata ya Kongowe na maeneo jirani.
Pamoja
na hilo, alialikwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kata ya Kongowe kuwa
Mgeni rasmi na amewapongeza Viongozi wote wanaomaliza muda wao, na
kuwahamasisha wanachama wenye nia wagombee kwa uadilifu Ili kuendelea
kukijenga na kukiimarisha chama .
Vilevile
amegawa vyeti kwa wanachama na Viongozi mbalimbali wa kata hiyo
waliofanya kazi za chama vizuri, akiwemo diwani viti maalum Kibaha,
Lidya Mgaya, vyeti ambavyo vilivyoandaliwa na Kamati ya siasa ya kata
hiyo ,:;Pia Koka amekabidhi viti 25 vya plastiki vyenye thamani ya Tsh
450,000/- kwenye mradi wa Vijana wa kata hiyo.

No comments:
Post a Comment